Majora Carter

Masimulizi ya Majora Carter kuhusu ustawi mpya wa miji

1,657,117 views • 18:36
Subtitles in 35 languages
Up next
Details
Discussion
Details About the talk
Transcript 35 languages
0:12

Iwapo uko hapa leo — nina furaha sana kwakuwa uko hapa — wote mmesikia kuhusu maendeleo endelevu yatatuokoa kutoka kwetu wenyewe. Lakini sisi hatuko TED, mara nyingi tunaambiwa kuwa ajenda ya sera ya maendeleo halisi si jambo linalowezekana, hasa katika miji mikubwa kama New York. Na mara nyingi ni kwa sababu watu wengi wenye uwezo wa kutoa maamuzi, katika sekta za umma na binafsi, hawaoni kama wako kwenye hatari.

0:38

Sababu ya kuwa hapa leo, pia, ni kwasababu ya mbwa: mtoto wa mbwa niliyemuokota kwenye mvua, mwaka 1998. Alikuja kuwa mbwa mkubwa zaidi ya nilivyotegemea. Wakati alipokuja kwenye maisha yangu, tulikuwa tunapinga sehemu kubwa ya jalala ambalo lilikuwa limepangwa kwa ajili ya ufukwe wa East River, pamoja na ukweli kwamba sehemu yetu ndogo ya jiji la New York tayari lilikuwa linapokea zaidi ya asilimia 40 ya uchafu wote unaotokana na shughuli za jiji. Sehemu ya kusafishia maji machafu, sehemu ya mafuta machafu, sehemu nne za umeme, sehemu kubwa kuliko zote duniani ya kusambaza chakula, pamoja na viwanda vingine ambavyo vinaingiza zaidi ya malori ya dizeli 60,000 katika sehemu hii kwa wiki. Eneo hili pia lina uwiano mdogo wa bustani za kupumzikia kwa ajili ya watu katika mji huu.

1:21

Kwa hiyo nilipofuatwa na kitengo cha bustani za kupumzikia karibu dola 10,000 za utekelezaji kusaidia kuendeleza miradi ya pwani. Nilifikiri walikuwa na heri, lakini hawajui kitu. Nimeishi eneo hili maisha yangu yote, na ulikuwa huwezi kufika mtoni kwasababu ya miundo mbinu ambayo niliyokwisha iongelea mwanzoni. Halafu, wakati nilipokuwa nakimbia na mbwa wangu asubuhi moja, alinivuta kwenye dampo ambalo nilifikiri kuwa liko hapo kimakosa. Kulikuwa na mizizi na rundo la uchafu na vitu vingine ambavyo sitavitaja hapa, aliendelea kunivutia kule — na lo na tazama, mwishoni wa rundo lile kulikuwa na mto. Nilijua kuwa huu mtaa mdogo uliosahauliwa, uliotupwa kama mbwa wangu aliyenileta hapaleo, ulikuwa na haki ya kusaidiwa. Na nilijua kuwa utakuja kuwa mwanzo wa kujivunia wa ufufuaji unaoendeshwa na jumuia mpya ya Bronx kusini.

2:01

Na kama ilivyo kwa mbwa wangu mpya, lilikuwa ni wazo ambalo lilikuwa zaidi ya nilivyofikiria. Tulipata msaada sana katika kuendeleza. Na bustani ya Hunts Point Riverside ilikuwa bustani ya pwani ya kwanza ambayo Bronx kusini ilikuwa nayo zaidi ya miaka 60. Tuliwezesha msaada wa dola 10,00 zaidi ya mara 300 kufikia bustani ya dola milioni 3.

2:18

Na wakati wa majira ya kupukutika majani, — Nitafunga ndoa na mpenzi wangu. Asante sana (Makofi). Ndio huyo hapo nyuma anayebonyeza kitufe, na hufanya hivyo mara zote. (Kicheko). (Makofi).

2:40

Lakini kwa sisi tunaoishi kwenye jumuia zinazojali mazingira ni canary katika machimbo ya makaa ya mawe. Tunayaona matatizo hayo sasa, na tumekuwa tukiyaona kitambo. Haki ya mazingira, kwa wale wanaoujua msemo huu, unasema kama hivi jumuia yeyote isibebeshwe mzigo wa mazingira na faida chache za mazingira kuliko nyinginge.

2:58

Kwa bahati mbaya rangi ya ngozi na class ni vielelezo vinavyonekana katika kupata vitu vizuri kama bustani za kuumzikia na miti, na mahali ambapo mtu anaweza kupata vitu vibaya, kama mitambo na sehemu za kutupia uchafu. Kama mtu mweusi nchini Marekani, nina uwezekano mara mbili kama mtu mweupe kuishi kwenye eneo ambalo uchafuzi wa hali ya hewa unaweza kuhatarisha afya yangu. Nina uwezekano mara tano wa kuishi karibu na mtambo au sehemu inayotoa kemikali hatari — ndiko ninakoishi. Haya maamuzi ya matumizi ya ardhi yametengeneza mazingira mabovu ambayo yanaleta matatizo kama ubwanyenye, kisukari na pumu. Nani anaweza kuondoka nyumbani kwake kutembea kwenye sehemu yenye kemikali za uchafu? Uwiano wetu wa ubwanyenye wa asilimia 27 ni mkubwa sana, hata kwa nchi hii, na kisukari kinakuja pamoja nayo. Mmoja kati ya watoto wanne wa Bronx kusini ana pumu. Uwiano wa watoto wanaolazwa kwa ajili ya pumu ni mkubwa mara saba zaidi ya asilimia ya nchi nzima. Matokeo haya yanakuja kwa njia tofauti. Na tunapata matatizo sana kwa ajili ya gharama za uchafu mgumu, matatizo ya afya yanayotokana na uchafuzi na kunuka zaidi, gharama ya kuwafunga vijana wetu weusi na wanaume wa kilatino, ambao wanauwezo mkubwa usioelezeka na ambao haujatumiwa ipasavyo. Asilimia 50 ya wakazi wetu wanaishi chini ya mstari wa umaskini. Asilimi 25 kati yetu hatuna kazi. Wananchi wanaopata kipato kidogo mara nyingi wanatumia vyumba vya dharura kama msingi. Hii inawaumiza walipa kodi na haitoi faida zilizosawa. Watu maskini sio tuu bado ni maskini, bado wana afya mbaya.

4:13

Kwa bahatio nzuri, kuna watu wengi kama mimi ambao wanataka kupata ufumbuzi ambao hautasumbua maisha ya jamii yenye kipato kidogo ya watu wa rangi kwa muda mfupi, na haitatuvuruga wote katika kipindi kirefu kijacho. Wote hatutaki hivyo, na wote tuna jambo linalofanana. Kwa hiyo tuna kitu gani kingine kinachofanana?

4:27

Kwanza, sote hapa tuna sura nzuri — (Kicheko)— tumemaliza sekondari, chuo, shahada za uzamili, tumesafiri sehemu zinazovutia, hatukupata watoto katika umri mdogo, kipato chetu ni kizuri, hatujawahi kufungwa. Sawa. Vizuri. (Kicheko).

4:44

Lakini, pamoja na kuwa mwanamke mweusi, niko tofauti na wengi wenu katika njia nyingine. Niliangalia karibu nusu ya majengo ya mtaani kwetu yakiungua. Kaka yangu mkubwa Lenny alipigana vita ya Vietnam, lakini aliuawa hatua chache kutoka nyumbani kwetu. Yesu. Nilikulia katika mtaa ambao ilikuwa mkabala na nyumba ya wavuta madawa ya kulevya. Ndio, mimi ni mtoto mweusi maskini kutoka geto. Vitu hivi vinanifanya niwe tofauti nanyi. Lakini vitu ambavyo tumefanana vinanitofautisha na watu wengi katika jumia yangu, na niko katika dunia hizi mbili, na moyo wangu wa kutosha wa kupigania haki katika jamii yangu.

5:20

Kwa hiyo ni jinsi gani vitu vimekuwa tofauti kwetu? Mwishoni mwa miaka ya 40s, baba yangu - mpagazi wa Pullman, mtoto wa mtumwa - alinunua nyumba huko Hunts Point sehemu ya Bronx Kusini, na miaka michache baadaye alimuoa mama yangu. Kwa miaka hiyo, wengi wa wanajumuia hiyo walikuwa wazungu, jumuia ya wafanyakazi. Baba yangu hakuwa peke yake. Na wengine kama yeye waliifata ndoto ya Marekani kwa jinsi wajuavyo wao, white flight ilikuwa kitu cha kawaida katika Bronx ya Kusini na miji mingine nchini. Red-lining ilikuwa inatumiwa na mabenki, katika baadhi ya maeneo ya jijini, ikiwa pamoja na kwetu, ilikuwa haijapewa kipaumbele kwa uwekezaji wa aina yeyote ile. Wenye nyumba wengi waliona ni faida zaidi kuchoma moto majengo yao na kupata hela za bima kuliko kuyauza yakiwa katika hali nzuri - bila kujali wapangaji wao kama wamekufa au kujeruhiwa.

6:03

Hunts Point ilikuwa ni jumuia iliyokuwa karibu na sehemu za kazi, lakini sasa wakazi hawana kazi wala nyumba za kwenda. Ujenzi wa barabara kuu uliongezwa kwenye matatizo yetu. Katika jimbo la New York, Robert Moses alichochea kampeni ya upanuaji wa barabara kubwa. Moja ya lengo lake kuu ilikuwa ni kuwarahisishia wakazi wa jumuia za matajiri huko katika kaunti ya Westchester kwenda Manhattan. Bronx Kusini, ambayo iko katikati, haikuwa na jinsi. Wakazi wa huko walipewa notisi ya chini ya mwezi mmoja kabla majengo yao hayavunjwa. Watu 600,000 walikosa makazi. Fikira za watu zilikuwa kwamba makuwadi, wauza madawa ya kulevya na malaya walikuwa wanatoka Bronx Kusini. Na kama unaambiwa toka mwanzo kuwa hamna kitu kizuri kinaweza kutoka katika jamuia yako, hiyo ni mbaya sana, itakuwaje isiakisi kwako? Kwa hiyo, nyumba yetu ilikuwa haina thamani, zaidi ya hilo ilikuwa ni nyumba yetu na tuliitegemea. Na kwa bahati kwangu, nyumba ile ilikuwa na upendo ndani yake pamoja nam saada kutoka kwa walimu, mentors na marafiki muda wote.

7:04

Sasa, kwanini hii hadithi ni muhimu? kwasababu ya mipango, kutetereka kwa uchumi kunasababisha uharibifu wa mazingira, ambao unasababisha mmomonyoko wa jamii. Kutokuwekeza kulikoanza miaka ya 1960 ndio kulikuwa msingi wa uharibifu wa mazingira ambao umekuja. Antiquated zoning na sheria za matumizi ya ardhi bado zinatumika mpaka leo kuendelea kuweka sehemu za uchafuzi wa mazingira katika maeneo yangu. Sababu hizi zinazingatiwa wakati sheria za ardhi zinapoamuliwa? Gharama ngapi zinahusiana na maamuzi haya? Na nani analipa? Nani anafaidika? Kuna kitu chochote kinachoonyesha matatizo ya jumuia? Hii ni "mipango" - katika mabano - ambayo haikuwa na manufaa kwetu katika fikra.

7:43

Mara tulipogundua hilo, tuliamua kuwa ni muda muafaka wa kupanga mipango yetu. Ile bustani ndogo ya mapumziko niliyowaelezea mwanzoni ilikuwa ndio hatua yetu ya kwanza ya kujenga a greenway movement katika Bronx ya Kusini. Niliandika moja na robo milioni federal transportation grant kusanifu mpango wa sehemu ya mapumziko ya ufukweni ambayo yana njia ya waendesha baiskeli Matengenezo yanasaidia kuhabarisha jamii kuhusu usalama barabarani, uwekaji wa uchafu na miundo mbinu mingine, ambayo kama itafanywa vizuri, haitahatarisha maisha ya wanajumuia. Inatoa fursa kwa jamii kujishughulisha, pamoja na maendeleo ya uchumi. Fikiria maduka ya baiskeli, viduka vya juisi. Tulipata dola milioni 20 za kuendeleza hatua ya kwanza miradi. Hapa ni Lafayette Avenue - na kama ilivyosanifiwa na wasanifu majengo wa Matthews-Nielsen. Na mara hii njia ikishajengwa, itaunganisha Bronx Kusini na zaidi ya ekari 400 za bustani ya mapumziko ya Randall's Island. Kwa sasa tunatenganishwa na karibu futi 25 za maji, lakini hiki kiunga kitabadilisha hayo.

8:33

Jinsi tunavyotunza mazingira asilia, ndivyo tutakavyofaidika zaidi. Tunaendesha mradi unaoitwa Bronx Ecological Stewardship Training, ambayo inasaidia kufundisha kazi katika maeneo ya ecological restorations, ili watu wa kutoka kwenye jumuia yetu wawe na uwezo wa kushindania hizi kazi zinazolipa vizuri. Kidogo kidogo, tunapandikiza mbegu za mafanikio katika maeneo yetu kwa ajili ya kazi nzuri - halafu watu watakuwa na maamuzi ya kifedha na binafsi kuhusu mazingira yao. Sheridan Expressway ni .......... ilijengwa bila kuzingatia mazingira yaligawanywa nayo. Hata wakati wa msongamano, ni wazi kwamba haitumiki sana. Jumuia ilitengenza mpango wa mbadala wa usafiri ambao uliruhusu kuondolewa kwa njia kubwa. Tuna fursa sasa ya kuwaunganisha wadau wote katika kufikiria hizi ekari 28 zinaweza kutumikaje vizuri kwa ajili ya Parkland, nyumba za bei nafuu na maendeleo ya uchumi.

9:20

Pia tumejenga jiji - paa la kwanza la kijani la jiji la New York mradi wa majaribio juu ya ofisi zetu. Paa nzuri ambazo hazinyonyi joto la jua na kuipitsha kwenye jengo au hewa. Paa za kijani ni udongo na mimea hai. Zote zinaweza kutumika badala ya vifaa vya kuezekea vyenye petroli ambayo inanyonya joto, inachangia katika matokeo ya urban "heat island" na kuharibu chini ya jua, ambayo tunaivuta. Paa za kijani pia zinatunza asilimia 75 ya mvua, kwa hiyo inapunguza mahitaji ya jiji kudhamini suluhisho la mabomba - ambayo, mara nyingi yamewekwa katika jumuia zisizo na haki ya mazingira kama yangu. Na nyumba ya rafiki zetu wadogo! Kwa hiyo — (kicheko) — nzuri sana! Hata hivyo, mradi wa mfano ni chanzo cha kuezeka paa zetu za kijani, kuongeza ajira na maendeleo endelevu katika Bronx Kusini. (Kicheko). (Makofi). Hata mimi napenda hiyo pia.

10:15

Hata hivyo, najua Chris alituambia tusijinadi hapa juu, lakini kwa kuwa mnanisikiliza: tunahitaji wawekezaji. Mwisho wa kujinadi. Ni afadhali kuomba msamaha kuliko ruhusa. Hata hivyo - (Kicheko). (Makofi).

10:33

OK. Katrina. Kabla ya Katrina, Bronx Kusini na wadi ya tisa ya New Orleans vina vitu vya kufanana. Yote ilikuwa na watu wengi wa jamii moja maskini, zote ni hotbeds za utamaduni ulioundwa: fikiria hip-hop na jazz. Zote ni jumuia za ufukweni ambazo zina viwanda wakaazi wanaokaa karibu karibu sana. Katika kipindi cha mpito cha Katrina, bado tuna vitu vya kufanana. Tunadharauliwa na kunyanyaswa sana, na negligent mashirika ya sheria, pernicious zoning and lax governmental accountability. Si uharibifu wa wadi ya tisa wala Bronx Kusini ulikuwa hauzuiliki. Lakini tumejifunza mengi jinsi ya kujinasua wenyewe. Tumekuwa zaidi ya nembo ya nchi ya bligh ya mjini. Au matatizo yatakayotatuliwa na ahadi za kampeni hewa za marais wanaokuja na waliopita. Sasa tutaacha pwani ya Gulf iteketee kwa muongo mmoja au miwili kama ilvyokuwa kwa Bronx Kusini? Au tutachukua hatua za ziada na kujifunza kutoka kwa wakereketwa ambao wametokana na jumuia yenye matatizo ka yangu?

11:33

Sasa sikiliza, sitegemei mtu binafsi, makampuni au serikali kuifanya dunia iwe mahali pazuri pa kuishi kwasababu ni sawa na sahihi. Hii presentation leo inaonyesha sehemu tuu ya mambo niliyopitia, sehemu ndogo tuu. Hujui. Lakini nitakuelezea baadae kama utapenda kujua. Lakini — najua ni shina, au jinsi mtu aonavyo, ndio kinachomchochea mtu mwishoni. Ninashauku na ninachopenda kuita "triple bottom line" ambayo maendleo endelevu yanaweza kuleta. Maendeleo ambayo yanaweza kuleta matokeo chanya kwa wahusika wote: waendelezaji, serikali na jumuia ambayo miradi hii inapelekwa. Kwa sasa hii haifanyiki katika jiji la New York. Na tunafanyakazi katika upungufu wa mipango miji madhubiti. Mlolongo wa ruzuku za serikali zinaenda kwenye miradi mikubwa iliyopendekezwa na ujenzi wa uwanja wa michezo katika Bronx Kusini, lakini kuna ushirikiano mdogo kati ya mashirika ya jiji na jinsi ya kabiliana na mkusanyiko wa matatizo ya foleni, uchafuzi wa hewa, uchafu na matokeo yake kwenye sehemu za wazi. Na mtazamo wao katika uchumi na kuendeleza ajira ni dhaifu sana hata si ya kuchekesha. Kwa sababu juu ya hilo, timu ya michezo tajiri sana duniani inachukua nafasi ya nyumba ambayo Ruth alijenga kwa kuvunja bustani mbili za jumuia za kupumzika ambazo zilipendwa sana. Sasa, tutakuwa na upungufu zaidi wa stat ambao niliwaelezea awali. Na ingawa chini ya asilimia 25 ya wakazi wa Bronx Kusini wana magari, miradi hii inajumuisha maelfu ya sehemu za kuegesha magari, bado fikiria kuhusu usafiri wa jiji Sasa, kipi kinakosekana kwenye mdahalo huu mkubwa ni mnyambulisho wa faida madhubuti kati ya na sio kurekebisha jumuia iliyo na mazingira yasiyo safi, dhidi ya majengo, mabadiliko endelevu. Shirika la ngu linafanya kazi kwa karibu sana na chuo kikuu cha Columbia na wengine ili kutoa mwanga kwa mabo haya.

13:18

Sasa hebu tuweke hii sawa. Mimi sipingi maendeleo. Sehemu yetu ni jiji, na sio hifadhi ya mbuga. Na nimeukumbatia ubepari ulio ndani yangu. Na siajabu wote mnayo pia ndani yenu, na kama hamna, mnahitaji kuwa nayo. (Kicheko). Kwa hiyo sina tatizo na waendelezaji kutengeneza pesa. Kuna precedent ya kutosha huko kuonyesha kuwa maendeleo endelevu ya jumuia bado yanaweza kuleta utajiri. Wenzangu wa TEDsters Bill McDonough na Emery Lovins — wote ni heros wangu - wameonyesha kuwa unaweza kufanya hivyo. Nina matatizo na maendeleo ambayo yanadidimiza jumuia zisizo na usemi kwa ajili ya faida. Hii ikiendelea ni aibu kwetu sote, kwasababu sote tunawajibika kwa maisha tunayoyatengeneza. Lakini kitu kimoja ninachofanya kujikumbusha juu ya uwezekano mkubwa ni kujifunza kutoka kwa wajuzi kwenye miji mingine. Haya ni maoni yangu juu ya utandawazi.

14:13

Hebu tuiangalie Bogota. Masikini, Latino, imezungukwa na wahalifu wenye silaha na uuzaji wa madawa ya kulevya: sifa si kama ile ya Bronx Kusini. Lakini, jiji lilibarikiwa mwishoni mwa miaka ya 1990 kwa kuwa na meya mwenye ushawishi aliyeitwa Enrique Penalosa. Aliangalia demographics. Wabogota wachaceh walikuwa na magari, lakini rasilimali kubwa ya jiji ilikuwa imetengwa kuwahudumia wao. Uwapo meya, waweza kufanya kitu fulani. Uongozi wake ulipunguza thoroughfares za manispaa kutoka njia tano mpaka tatu, ikapiga marufuku kupaki katika mitaa hiyo, ikapanua njia za watembea kwa miguu na barabara za waendesha baiskeli, ikatengeneza public plazas, ikatengeneza eficient buss mass-transit systems katika dunia nzima. Kwa juhudi zake nzuri, alikuwa karibu avuliwe madaraka. Lakini jinsi watu walivyoanza kuona kuwa wao wanapewa kipaumbele kwenye masuala mbalimbali yanayohusu shughuli zao za kila siku, mambo mazuri yakatokea. Watu waliacha kutupa taka ovyo. Uhalifu ulipungua. Kwasababu mitaa ilikuwa imejaa watu. Uongozi wake ulipigana na matatizo mbalimbali ya mijini moja baada ya jingine, na katika bajeti ya dunia ya tatu. Hatuna visingizio kwenye nchi hii. Samahani. Lakini cha muhimu ni, ajenda yao ya kuwaweka watu kwanza haikumaanisha kuwapiga faini wale wasio kuwa na uwezo wa kuwa na magari, bali kutoa fursa kwa wabogota kushiriki katika maendeleo ya jiji. Maendeleo hayo yasije kwa expense ya walio wengi hii bado inaonekana kama ni wazo zito sana hapa Marekani. Lakini mfano wa Bogota una nguvu ya kubadili hili.

15:43

Ninyi, mmebarikiwa na zawadi ya ushawishi. Hii si sababu kwanini mko hapa na kwanini mna thamini hizi habari tunazobadilishana. Tumieni utashi wenu kuunga mkonomabadiliko endelevu madhubiti kila mahali. Msiongelee tuu kuhusu haya kwenye TED. Hii ni agenda ya nchi nzima ninayojitahidi kuijenga, na kama mjuavyo, siasa ni kitu cha binafsi. Nisaidieni kufanya kijani iwe nyeusi mpya. Nisaidieni kufanya uendelevu uwe wa kuvutia. Fanyeni yawe mazungumzo yenu wakati wa chakula cha usiku na wakati wa sherehe. Nisaidieni kupigania haki ya mazingira na uchumi. Ungeni mkono uwekezaji wenye kulerta faida mara tatu. Nisaidieni kuleta demekrasia katika uendelevu kwa kuhusisha kila mtu katika hili na kusisitiza mpango madhubuti unaweza kuongelewa kila mahali. Oh vizuri, afadhali nina muda kidogo!

16:28

Sikiliza - nilipoongea na Bw. Gore juzi baada ya kifungua kinywa, nilimuuliza wakereketwa wa haki za mazingira watawekwa wapi katika mkakati wake mpya. Jibu lake lilikuwa ni programu ya misaada. Sidhani kama alielewa kuwa nilikuwa siombi msaada. Nilikuwa nampa ofa. (makofi).

17:01

Kilichonisumbua ni kwamba huu mtazamo wa juu-chini bado upo. Sasa, msinielewe vibaya, tunahitaji pesa. (kicheko). Lakini vikundi vya grassroots vinahitajika wakati wa kufanya maamuzi. Kati ya asilimia 90 ya nguvu tunazopoteza kila siku ambayo Bw. Gore alitukumbusha, hajumuishi kupoteza nguvu zetu, akili na ujuzi wetu mkubwa. (makofi).

17:34

Nimetoka mbali kukutana nanyi kama hivi. Tafadhali msinipoteze. Kwa kufanya kazi pamoja, tunaweza kuwa moja ya vikundi vidogo vinavyokuwa haraka ambao wana ujasiri na ushujaa wa kuamini kuwa tunaweza kubadili dunia hii. Tumekuja kwenye kongamano hili kutoka kwenye sehemu tofauti za maisha, lakini naamini, wote tunashirikiana kwa kitu kimoja kikubwa — hatuna cha kupoteza na tunaweza kupata kila kitu. Kwaheri Wapendwa! (Makofi)

Katika mhadhara uliojaa hisia, mwanaharakati mshindi wa tuzo ya MacArthur, Majora Carter anaelezea kuhusu mapambano yake kutetea haki za kimazingira huko Bronx Kusini — na anaonyesha namna ambavyo maeneo ya miji waishiko wanyonge wachache yanaathirika kutokana na sera mbovu za mipango ya miji.

About the speaker
Majora Carter · Activist for environmental justice

Majora Carter redefined the field of environmental equality, starting in the South Bronx at the turn of the century. Now she is leading the local economic development movement across the USA.

Majora Carter redefined the field of environmental equality, starting in the South Bronx at the turn of the century. Now she is leading the local economic development movement across the USA.