Alichonifundisha Adui Wangu Mbaya Sana Kuhusu Moyo wa Shukrani
509,867 views |
Jim Enderle |
TEDxBismarck
• August 2021
Nikiwa nimepelekwa Iraki kama Askari wa Afya wa Jeshi la maji, mpiganaji wa Al-Kaeda tuliyemweka kizuizini alibainisha kuwa kwa namna flani alipata bahasha iliyokuwa na anuani ya familia yangu. Katika machafuko ya shambulizi za roketi na mizinga, nilikwenda kumkabili lakini nikamkuta katika dakika zake za mwisho badala yake. Karibu sana kiasi cha kusikia kupumua kwa kila mmoja, tulisimama pale, nyuso zetu zikilainika kabla hajafariki. Baadaye, nilimwuliza mkalimani wangu kama ningeweza kufahamu zaidi kuhusu mpiganaji yule na akatoa barua zilizotafsiriwa kati yake na watu wapendwa wake. Baada ya kipindi kigumu cha mpito kurudi nyumbani baada ya vita kilichosababisha kutengana na familia na matatizo mengine, nilianza kusoma zile barua katika shauku kubwa ya kuyaweka maisha yangu katika mpangilio. Kama njia ya maisha mazuri zaidi ingetolewa na maridhiano yangehakikishwa, ningesikiliza kama njia hii ingetokea kwa adui wangu mkubwa?