Ingekuwaje kama gharama za afya Marekani zingekuwa wazi?
2,096,818 views |
Jeanne Pinder |
TED Residency
• December 2018
Marekani, kipimo cha damu cha kimoja, kinaweza kugharimu $19 katika kliniki moja na $522 katika kliniki nyingine majengo machache baadaye -- na hakuna ajuaye tofauti mpaka baada ya wiki moja wanapopata bili. Mwanahabari Jeanne Pinder anasema haihitaji kuwa hivi. Alijenga jukwaa ambalo linakusanya taarifa za gharama halisi za huduma za afya na kuweka taarifa wazi kwa wote, likifichua siri za bei za huduma za afya. Jifunze jinsi kujua gharama za vitu mapema kunavyoweza kutufanya tuwe na afya zaidi, na kuokoa pesa -- na kusaidia kurekebisha mfumo mbovu.