Ishi kama unakufa? Kutenda katika mashaka | Ariel Dempsey | TEDxMSU
11,971 views |
Ariel Dempsey |
TEDxMSU
• March 2020
Linapokuja suala la kufuatilia maono yetu, ni rahisi kuhisi kushindwa kufanya kitu kutokana na mashaa; tunawezaje kupata ujasiri wa kutenda, hata pale tusipoweza kuona?
Ariel Dempsey shares a story she has kept secret from many: her story of receiving a terminal diagnosis and recovering from traumatic brain injury. As a medical student at Michigan State and a PhD student in science and religion at Oxford, she draws on both medicine and spirituality to reflect on living with uncertainty. She embodies her message in a beautiful and inspiring performance danced in aerial silks.
Ariel Dempsey ni mwanafunzi wa mwaka wa nne wa udaktari ambaye anakaribia kuhitimu kutoka chuo kikuu cha Jimbo la Michigan akiwa na shahada ya Udaktari na akielekea kukamilisha shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika sayansi na dini katika chuo kikuu cha Oxford. Anatazamia kuwa daktari wa kuhudumia watu wasiojiweza akihusisha elimu ya udaktari na ya dini. Ukiacha masomo yake, Ariel anapenda dansi la kuzunguka angani na sanaa ya sarakasi. Ni sehemu ya kikundi huko Grand Rapids kiitwacho Bangarang Circus na amesafiri pwani ya California akitumbuiza mitaani kuchangisha pesa kwa ajili ya kusaidia shirika la WorldVision na kuchangisha pesa kwa ajili ya huduma za Afya.
Mazungumzo haya yalifanyika katika tukio la TEDx kwa kutumia muundo wa mkutano wa TED lakini likiandaliwa na jamii ya watu wa eneo husika. Jifunze zaidi hapa https://www.ted.com/tedx