Stephen Cave

Hadithi nne tunazoambia nafsi zetu kuhusu kifo

2,238,008 views • 15:33
Subtitles in 33 languages
Up next
Details
Discussion
Details About the talk
Transcript 33 languages
Translated by Nelson Simfukwe
Reviewed by Joachim Mangilima
0:11

Nina swali: Ni wakina nani hapa walishawahi tambua lini watakufa?

0:20

Natambua.Nilikuwa mvulana mdogo, na babu yangu alikuwa amefariki, na nakumbuka siku chache baadaye nikiwa nimelala kitandani wakati wa usiku nikijaribu kujiuliza kipi kilichotokea. Ilimaanisha nini kwamba amekufa? Atakuwa ameenda wapi? Ilikuwa ni kama shimo limefunguka na likammeza. Na swali la kushtua likanijia: Kama amekufa,inaweza ikanitokea na mimi? Hilo shimo litafunguka na kunimeza? Litafunguka chini ya kitanda changu na kunimeza wakati nimelala? Katika namna fulani,watoto wote wanakuja gundua kuhusu kifo. Kinaweza kutokea katika njia nyingi tofauti, na kawaida huja kwa hatua. Mawazo yetu kuhusu kifo yanakua kadiri tunavyozidi kuzeeka. Na kama ukifika katika kona za giza za kumbukumbu yako, utakumbuka kitu fulani kama nilichohisi mimi wakati babu yangu alipofariki na nilipogundua inaweza kunitokea na mimi pia, hiyo maana iliyopo nyuma ya haya yote ubatili unangojea.

1:27

Na haya maendeleo katika utoto yanaakisi maendeleo ya aina yetu. Kama kulivyokuwa na alama katika maendeleo yako kama mtoto wakati utambuzi wako wa nafsi na muda ulivyokuja kuchanganyika vya kutosha kiasi cha wewe kutambua haitaishi milele, kwa hiyo katika hali fulani ya mabadiliko yetu, baadhi ya utambuzi wa binadamu wa nafsi na muda ukaja jichanganya vya kutosha. kwa wao kuja kuwa binadamu wa kwanza kutambua, "naelekea kufa" Kama unapenda,laana yetu. Ni gharama tunayolipa kwa kuwa werevu wajinga. Tunatakiwa kuishi katika maarifa hicho ni kitu kibaya kinachoweza kutokea siku moja kwa uhakika, mwisho wa miradi yetu, matumaini yetu,ndoto zetu,katika dunia ya kila mmoja. Tunaishi katika kivuli cha kuwaza mwisho wa dunia.

2:24

Na inaogopesha.Na kutisha. Kwa hiyo tunatafuta njia ya kujinasua. Kwa upande wangu,nilipokuwa na miaka mitano, hii ilimaanisha kumuuliza mama yangu. Sasa nilipoanza kuuliza kipi kinatokea tukifarikia, watu wazima waliokuwa wananizunguka wakati huo walijibu katika mchanganyiko wa kiingereza na ulio mgumu kuelewa. na mkristo mwenye nusu moyo, na kipande cha sentensi ninachosikia mara nyingi ilikuwa kwamba babu kwa sasa "yuko juu akituangalia sisi" na kama nikifa pia, na mimi pia nitaenda juu, hiki kinafanya kifo kionekane kama lifti isiyoonekana kwa macho lakini inafanya kazi. Lakini hii haikuonekana kama ina ukweli sana. Nilizoea kuangalia habari za watoto wakati huo, na huu ulikuwa wakati wa kujifunza kuhusu unajimu. Kulikuwa na roketi zinakwenda juu angani, zinakwenda huko. Hamna mnajimu ambaye alirudi na akasema kwamba amekutana na babu yangu au mtu yoyote aliyekufa. Lakini nilikuwa naogopa, wazo la kupanda lifti ya kifo kumuona babu yangu naona ni bora zaidi kuliko kwenda kumezwa wakati nimelala. na nikaamini, pamoja haikuleta maana sana.

3:40

Na hili wazo nililokuwa nalo wakati nikiwa mtoto,nimekuwa nalo kwa muda sana hadi nikiwa mtu mzima, ni zao ambalo wanasaikolojia wanaita upendeleo. Sasa upendeleo ni njia ambayo hufanya vitu kimakosa, njia ambazo tunakosea kukokotoa,kutoa maamuzi, kuharibu uhalisia,au kuona tunachotaka kuona, na upendeleo ninaoongelea unafanya kazi kama hivi: Kumfata mtu na ukweli kwamba atakufa na wataamini kuhusu hadithi yoyote ambayo inawaambia sio kweli na badala yake,wanaweza kuishi milele, hata kama inamaanisha watapanda lifti. Sasa tunaweza kuona huu ni upendeleo kupita wote. Imeelezew katika zaidi ya masomo 400 ya undani. masomo haya ni ya werevu,lakini ni rahisi. Yanafanya kazi kama hivi. Unachukua makundi mawili ya watu ambao wako sawasawa katika kila kitu, na unawaambia kundi moja kwamba watafariki wengine huwaambii,unalinganisha tabia zao. Kwa hiyo unaangalia jinsi gani unafanya tabia zao kuwa watu wanapoanza kugundua kuhusu vifo vyao. Na kila wakati,unapata matokeo yaleyale: Watu ambao tayari washatambua kuhusu vifo vyao wako tayari kuamini hadithi ambazo zinawaambia wanaweza kukwepa kifo na kuishi milele. Huu ni mfano:Tafiti moja ya hivi karibuni ilichukua makundi mawili ya wapagani, hao ni watu ambao hawana maamuzi katika kuamini dini. Sasa,kundi moja liliambiwa kufikiria kuhusu kufa. Kundi lingine likaambiwa kufikiria kuhusu kuwa mpweke. Waliulizwa tena kuhusu imani zao za kidini. Wale walioambiwa kufikiria kuhusu kifo walikuwa wakielezea mara mbili zaidi hisia zao kuhusu Mungu na Yesu. Mara mbili zaidi. Pamoja na kwamba wote walikuwa wapagani. Lakini weka uoga wa kifo ndani yao, watakimbila kwa Yesu.

5:40

Sasa,hii inaonesha kwamba kuwakumbusha watu kuhusu kifo inawachochea kuamini,bila kujali ukweli, na sio kwa dini tu, katika imani yoyote ile ambayo inaeleza kifo katika njia tofauti tofauti, haijalishi kama inakuwa maarufu au kuwa na watoto au utaifa, ambayo inasema utaishi siku zote. Huu ni upendeleo uliotengeneza umbile na historia y binadamu.

6:08

Sasa,fikra iliyopo katika upendeleo huu katika tafiti 400 inaitwa fikra ya usimamizi wa uoga, na wazo ni rahisi.Ni hivi. Tunakuza mawazo yetu kuhusu dunia, hivyo,hadithi tunazoambia nafsi zetu kuhusu dunia na sehemu yetu ili kusaidia kusimamia hofu ya kifo. Na hizi hadithi za kifo zina maelfu ya shuhuda tofauti tofauti, lakini naamini nyuma ya utofauti uliopo kuna aina nne za muhimu ambazo hizi hadithi za vifo zinahusiana. Na tunaweza kuona zinajirudia katika historia,na utofauti mdogo sana kuakisi msamiati wa siku. Sasa nitatoa muhtasari wa hizi aina nne kuu za hadithi za kifo, na ninataka kujaribu kukuonesha maana ni jinsi gani vinaelezewa kwa kuirudia katika kila utamaduni au kizazi kwa kutumia msamiati wa siku.

7:04

Sasa,hadithi ya kwanza ni rahisi sana. Tunataka kukwepa kifo, na ndoto ya kufanya hicho katika mwili huu katika hii dunia milele ni hadithi ya kwanza na rahisi ya kifo, na inaweza kuonekana isiyo na maana kwa mara ya kwanza, lakini kiukweli,karibia kila tamaduni katika historia ya binadamu ilikuwa na mzimu au kiongozi mkongwe wa kutupa maisha au kurudisha wazee katika ujana au kitu kinachotuahidi sisi kuendelea mbele milele. Wahenga wa Kimisri walikuwa na huo mzimu, Wahenga wa Babylon,wa India. Katika historia ya ulaya,tunawaona katika kazi ya wanakemia wa kizamani, na mpaka leo tunaamini, tunahdithia hizi hadithi kwa kutumia msamiati wa sayansi. Miaka 100 iliyopita, homoni zilikuwa zimegunduliwa, na watu wakatumaini kwamba matibabu ya homoni yatatibu uzee na magonjwa, na sasa tunaweka matumaini yetu katika kiini shina uhandisi wa gene,na teknolojia ya nano. Lakini wazo kwamba sayansi inaweza kuponya kifo liko sura moja mbele zaidi katika hadithi ya maajabu ya kuweza kuishi milele, hadithi ambayo ni ya zamani kama ulivyo ustaarabu. Lakini kuweka mawazo yote katika kufikiria kutafuta kuishi milele na kukaa wazima siku zote ni mkakati wenye hatari sana. Tukiangalia nyuma katika historia wale waliotafuta kuishi milele huko nyuma, kitu kimoja ambacho wote wanacho ni kwamba wote wameshakufa.

8:28

Kwa hiyo tunahitaji mpango wa kutukomboa,na mpango huu mbadala ni ambao aina ya pili ya kifo inaelezea, ni kufufuka. Na hiyo inakuwa ni wazo kwamba mimi ni huu mwili, Ni kiumbe kamili. Kinakubali kwamba kitakufa lakini kinasema,pamoja na hilo, Ninaweza amka na nikaishi tena. Katika maneno mengine,naweza fanya kama alichofanya Yesu. Yesu alikufa,akakaa siku tatu kaburini, na baada ya hapo akafufuka na kuamka tena. Na wazo ambalo tunaishi nalo ni kwamba wote sisi tunaweza fufuka na kuishi tena hata waimani ya Orthodox wanaamini,si kwa wakristo tu hata Wayahudi na Waislamu. Lakini tamaa yetu katika kuamini hizi hadithi imefungamana kiundani sana kwamba tunaivumbua tena kwa enzi za kisayansi, kwa mfano,kwa kutumia wazo la kutumia mazingira ya joto dogo sana ili kuweza kutunza kiumbe kirudi katika uhai Wazo ni kwamba ukifa, unaweza kujigandisha mwenyewe, na baadaye,katika namna fulani teknolojia imekua vya kutosha, unaweza kutengenezwa na tena kurudi katika uhai kwa kufufuka. Na watu wanaamini Mungu wa nguvu zote atawafufua na wataishi tena, na wengine wanaamini wanasayansci wenye nguvu na maarifa watawafufua nao pia.

9:34

Lakini kwa wengine,wazo zima ni kuhusu kufufuka, kwa kutoka nje ya kaburi, ni kama zile sinema z kutisha za zombies. Mwili unakuwa mchafu sana,usiotamanika kwa kuwezesha maisha ya milele, Watu wanaweka matumaini yao katika hili swala la tatu, hadithi ya kifo iliyokaa kiroho zaidi, wazo kwamba tutaiacha miili yetu nyuma na kuishi kama roho. Sasa,watu wengi katika dunia wanaamini wana roho, na wazo hili ni kuu kwa dini nyingi. Lakini hata hivyo,katika mfumo wa sasa, katika utamaduni wake, wazo la roho ni maarufu sana, achilia yote hayo tunakuja tena kuvumbua wazo hili katika nyakati za kidigitali, kwa mfano unaweza kuacha mwili wako nyuma kwa kuwezesha akili yako,uhalisia wako, wewe halisi,kwenye kompyuta, na kuishi kama avatar.

10:24

Lakini kuna wabishi ambao wanasema tukiangalia katika ukweli wa sayansi, hasa sayansi ya mishipa ya fahamu, inadokeza kwamba,akili yako uhalisi wako, vinategemea sana upande fulani wa mwili wako,ambao ni ubongo. Na aho wenye wasiwasi wanaweza pata faraja katika aina ya nne ya hadithi ya kifo, na huo ni urithi, wazo kwamba unaweza ishi mpaka kwenye mwangi unaiacha dunia, kama mwanajeshi hodari wa Kigiriki Achilles, aliyetoa sadaka ya maisha yake kwa Troy ili kupata umaarufu wa kifo. Na umaarufu ulisambaa na ni maarufu kama ilivyokuwa zamani, na katika nyakati hizi za kidigitali, ni rahisi sana kufanikiwa. Huitaji kuwa kama mwanajeshi hodari kama Achilles au kuwa mfalme hodari au shujaa. Unachohitaji ni mtandao wa intaneti na paka anayefurahisha(Vicheko) Lakini watu wengi wanapendelea kuacha vile vionekanavyo, urithi wa kibiolojia—watoto,kwa mfano. Au wapo hivi,wana imani,kuishi katika nafasi ya maisha yote, taifa au familia au kabila, gene zao. Lakini tena,wanakuwa na wasiwasi wana wasiwasi kwamba urithi kiuhalisia ni kuhusu kifo. Kwa mfano,Woody Allen alisema, "Sitaki kuishi katika mioyo ya watu wa nchi yangu. Nataka kuishi katika nyumba yangu"

11:39

Hizo ni aina nne kuu za hadithi za kifo, na nimejaribu kuonesha maana ni jinsi zinasemwa na kila jamii na utofauti mdogo sana kutosha fasheni ya siku. Na ukweli kwamba zinajirudia katika hii njia, katika mfumo uleule lakini katika aina tofauti za kuamini, Nadhani, tunatakiwa kuwa na wasiwasi wa ukweli katika aina yoyote ya hadithi hizi. Ukweli kwamba watu wanaamini mungu mwenye nguvu atawafufua na kuishi tena na wengine wanaamini wanasayansi wenye nguvu watawafufua na kuishi tena. inasema kwamba hamna anayeamini hili au nguvu ya ukweli. ila,tunaamini hadithi hizi kwa sababu tunachochewa kuziamini, na tunachochewa kuziamini kwa sababu tunaogopa kifo.

12:30

Kwa hiyo swali ni, je,tunapotoshwa kuongoza maisha tuliyonayo katika njia ya uoga na kupotosha ukweli? au tunaweza kushinda huu uchochezi? Mphilosophia wa kigiriki Epicurus alifikiri tunaweza. Alihoji kwamba uoga wa kifo ni kitu cha asili, lakini sio cha mantiki. "kifo",alisema,"si kitu kwetu, kwa sababu tuko hapa,kifo hakipo, na wakati kifo kikiwa hapa,na sisi tunakuwa hatupo" Mara nyingi kauli hii huwa inanukuliwa,lakini ni vigumu kuielewa,kiundani zaidi, kwa sababu kiuhakika wazo hili la kuondoka ni gumu sana kulifikiria. Miaka 2000 baadaye,mphilosophia mwingine, Ludwig Wittgenstein,alisema: "Kifo sio tukio la maisha: Hatuishi ili kuzoea kifo. Akaongeza kwa kusema, "katika maana hii,maisha hayana mwisho"

13:26

Kwa hiyo ilikuwa halisi kwa mimi kama mtoto kuogopa kumezwa na shimo la kifo, lakini haikuwa na mantiki, kwa sababu kumezwa na shimo la kifo sio kitu ambacho mtu yoyote kati yetu ataishi na kukutana nacho.

13:41

Sasa,kukwepa uchochezi huu sio kitu rahisi kwa sababu hofu ya kifo imo ndani yetu, wakati huohuo tunaona uoga huna mantiki, na tunapoonyesha uoga katika njia ambazo tunachochewa bila kujitambua, angalau tunaweza kuanza kupunguza ule msukumo ulionao katika maisha yetu.

14:02

Sasa,naona inasaidia kuona maisha ykifanana na kama kitabu: Kama kilivyozungukwa na kava, mwanzoni na mwishoni, kwa hiyo maisha yetu yamezungukwa kwa kuzaliwa na kifo, na hata kama kitabu kina mipaka mwanzoni na mwishoni, inaweza jumuisha mazingira ya mbali, maumbile ya kusisimua,matukio mazuri sana. Na hata kama kitabu kina mipaka mwanzoni na mwishoni, wahusika ndani yake hawajui mwisho wa upeo wa macho. Wanajua nyakati zinazohusu hadithi zao, hata kama kitabu kikifungwa. kwa wahusika katika kitabu hawaogopi kufika ukurasa wa mwisho. Long John Silver hakuogopi kumalizia nakala yako ya "Treasure Island" na itakuwa na sisi. Fikiria kitabu cha maisha yako, inakava,mwanzoni na mwishoni,kuzaliwa kwako na kufa kwako. Unaweza kujua nyakati, zinazofanya maisha yako. Haileti maana kwa wewe kuogopa kilicho nje ya kava, kama ni kabla ya kuzaliwa au baada ya kifo chako. Na hautakiwi kuwa na wasiwasi kitabu ni kirefu kiasi gani, au ni cha kichekesho au kinaelezea ukubwa wa kitu. Kitu kimoja cha msingi ni kwamba unaifanya iwe hadithi nzuri.

15:18

Asante.

15:20

(Makofi)

Mwanaphilosophia Steven Cave anaanza kwa swali lenye kazi lakini la kulazimisha kufikiria:Lini ulitambua utakuja kufa?Na cha kusisimua zaidi:Kwa nini wanadamu huwa tunakwepa kifo?Katika hotuba hii ya kuvutia Bwana Cave anachambua vitu vinne katika maisha ya binadamu ambapo huwa tunaambia nafsi zetu "ili kutusaidia kupambana na uoga wa kifo"

About the speaker
Stephen Cave · Philosopher

Philosopher Stephen Cave wants to know: Why is humanity so obsessed with living forever?

Philosopher Stephen Cave wants to know: Why is humanity so obsessed with living forever?