Sonia Shah

Sababu tatu kwa nini hatujaitokomeza malaria

1,111,128 views • 15:18
Subtitles in 28 languages
Up next
Details
Discussion
Details About the talk
Transcript 28 languages
Translated by Nelson Simfukwe
Reviewed by Joachim Mangilima
0:11

Kwa muda mrefu katika historia ya mwanadamu, ugonjwa wa kuambukiza ambao umeua wanadamu wengi kuliko mwingine ni malaria. Unabebwa katika ving'atio vya mbu, na inawezekana ni janga letu la muda mrefu. Inawezekana tulikuwa na malaria tangu tulipotokea kwenye enzi za sokwe. Na mpaka leo,malaria inachukua inasababisha madhara makubwa katika jamii yetu. Malaria inagundulika mara milioni 300 kwa mwaka na vifo vipatavyo nusu milioni

0:38

Sasa,hii haiingii akilini kabisa. Tumejua jinsi ya kutibu malaria tangu mwaka 1600. Wakati huo wamissionari wa Peru waligundua gamba la mti wa cinchona, na ndani ya gamba hilo kulikuwa na quinine, ambayo ndiyo tiba ya malaria mpaka leo. Kwa hiyo tumejua jinsi ya kutibu malaria kwa karne sasa. Tumejua jinsi ya kuzuia malaria tangu mwaka 1897. Ambapo ndiyo kipindi ambacho daktari mwanajeshi wa Kiingereza Ronald Ross aligundua kwamba alikuwa ni mbu ambaye anaambukiza malaria, sio hewa chafu au anga chafu ,kama ilivyokuwa ikifikiriwa mwanzoni. Kwa hiyo malaria inatakiwa iwe ni gonjwa rahisi kutibu, lakini mpaka leo,mamia ya maelfu ya watu wanakufa kutokana na kung'atwa na mbu. Kwanini iwe hivyo?

1:25

Hili ni swali ambalo binafsi limenifanya niwe mdadisi kwa muda mrefu. Nimelelewa na wazazi wahamiaji wa kutoka India nikiwatembelea mabinamu zangu nchini india kila kiangazi, na kwa sasa sikuwa na kinga ya malaria, Nilikuwa nalala kwenye chandarua chenye joto sana kila siku wakati binamu zangu,waliruhusiwa kulala nje kwenye mitaro na kupata hewa nzuri ya usiku. Na nilichukia sana mbu kwa hilo. Lakini wakati huohuo,nilitokea katika familia ya Jain, na dini ya jaini inaunga mkono sana aina ya kutofanya fujo. Watu wa dini ya jain hawaruhusiwi kula nyama. Hatutakiwi kutembea kwenye nyasi, kwa sababu unaweza kuua wadudu unapotembea kwenye nyasi. Haturuhusiwi kuwaua mbu. Uoga wa kumuogopa mdudu huyu mdogo ulianza tangu nilipokuwa na umri mdogo, na ndiyo sababu kwanini nimetumia miaka mitano kama mwandishi wa habari nikijaribu kuelewa,kwanini malaria imekua adui mbaya sana kwetu sote kwa muda mrefu? Na nafikiri kuna sababu kuu tatu ni kwanini. Hizo sababu tatu zinaingizwa kwenye sababu ya nne, ambayo inawezekana ndiyo sababu kubwa kuliko zote.

2:35

Sababu ya kwanza ni ya kisayansi. Mdudu huyu mdogo anayesababisha malaria, ni mmoja wa vijidudu watata wanaojulikana kwa mwanadamu. Anaishi nusu ya maisha yake katika mbu mwenye damu baridi na nusu nyingine ndani ya binadamu mwenye damu vuguvugu. Haya mazingira mawili ni tofauti kabisa, lakini si hivyo tu,yana uhamasa mkubwa sana. Kwa hiyo mdudu anaendelea kujaribu kupambana na vimelea, na binadamu nae anaendelea kupambana na vimelea. Mdudu anaendelea kuishi pamoja na mashambulizi haya,, sio tu anaishi,anastawi pia. Amesambaa.Ana njia nyingi za kukimbia kushambuliwa zaidi ya tunavyojua. Huwa vinabadili umbo,kwa kitu kimoja Kama vile funza anavyobadilika kuwa kipepeo, vimelea vya malaria vinajibadili kwa aina hiyo mara saba katika maisha yake. Na hatua hizo zote za maisha sio tu zipo tofauti, zina mfumo wa tofauti kabisa. Kwa hiyo tuseme unagundua dawa nzuri sana ya kutibu inayopambana na hatua moja ya maisha ya vimelea hivi. Haitafanya kazi katika hatua nyingine yoyote. Vitajificha kwenye miili yetu,bila kugundulika, bila kujulikana ,kwa siku,kwa wiki kadhaa, kwa miezi,kwa miaka,na wakati mwingine hadi kwa miongo.

3:52

Kwa hiyo vimeleani changamoto kubwa sana kuishinda, mbu ambaye ndiye anaambukiza malaria. aina 12 tu za mbu zinabeba malaria yanayoambukizwa duniani na tunajua kidogo tabia ya umajimaji waliyozoea Kwa hiyo unaweza fikiria,kwanini tusiepukane na sehemu ambazo mbu wanaishi?Sawa? Tunaweza epuka wanapoishi dubu na tunaweza epuka sehemu ambapo mamba anaishi. Lakini tuseme unaishi kwenye maeneo ya tropiki na unatoka nje ya tembe yako siku moja na unaacha alama za miguu kwenye uchafu laini karibu na nyumbani kwako. Au tuseme ng'ombe wako kafanya hivyo,au nguruwe kafanya hivyo, na baadaye mvua ikanyesha, na hizo alama za miguu zikajaa maji. Unakuwa umetengeneza makazi mazuri sana nje ya nyumba yako. Inakuwa sio rahisi kuondokana na mbu. Tunatengeneza sehemu wanazopendelea kuishi kwa kuishi maisha yetu.

4:51

Kwa hiyo kuna changamoto kubwa sana ya kisayansi lakini kuna changamoto kubwa sana ya kiuchumi. Malaria inatokea katika sehemu masikini sana na sehemu za nje ya miji duniani, na kuna kwa hilo. Kama wewe ni masikini,una uwezekano mkubwa wa kupata malaria. Kama wewe ni masikini,una uwezekano mkubwa wa kuishi katika makazi duni katika ardhi ambayo ni yenye madimbwi mengi. Hizi ndizi sehemu ambapo mbu wanazaliana. Uwezekano wa kuwa na nyavu za mbu milangoni na madirishani unakuwa mdogo. Uwezekano wa kuwa na umeme, unakuwa mdogo. na shughuli zote ambazo zinawezeshwa na umeme ndani ya nyumba, unakuwa upo nje zaidi. Unang'atwa na mbu.

5:24

Kwa hiyo tunaona umasikini unasababisha malaria, lakini tunajua sasa kwamba malaria yenyewe inasababisha umasikini. Kwa kitu kimoja,huwa inakumba muda wa mavuno, muda uleule ambapo wakulima wanakuwa mashambani kuvuna mazao yao,wanakuwa nyumbani wakiumwa homa. Lakini pia inawaweka watu katika hatari ya kifo kutokana sababu nyingine zote. Hili limetokea kihistoria. Tumeweza kuondoa malaria kwa jamii. Kila kitu kinabaki vilevile, tuna chakula kibaya,maji yasiyo salama,mazingira bora, na haya yote yanasababisha watu kuumwa. Lakini kama utaondoa malaria, vifo kutokana na sababu nyingine vitapungua. Na mwanauchumi Jeff Sachs ameonesha hii ina maana gani kwa jamii. Inachomaanisha ni kwamba,kama una malaria katika jamii yako, ukuaji wako wa uchumi unadidimia kwa asilimia 1.3 kila mwaka, mwaka baada ya mwaka,kwa hili gonjwa moja tu. Hii inaleta changamoto kubwa sana ya kiuchumi, kwa sababu unasema umeleta dawa bora au chanjo bora— unaitoa vipi kwenye sehemu ambazo hazina barabara, hazina miundombinu, hazina umeme kwa kugandisha vitu kwenye jokofu, hazina zahanati,hazina wataalamu wa afya. kutoa huduma hizi zinapohitajika Kwa hiyo kuna changamoto kubwa katila kupambana na malaria.

6:42

Lakini pamoja na changamoto ya kisayansi na changamoto ya kiuchumi, kuna changamoto ya kitamaduni pia, na hii moja ya upande wa malaria ambayo watu hawapendelei kuiongelea. na ni mkanganyiko kwamba watu wenye malaria sana duniani wanalichukulia hawajali kwa uzito. Haya yamekuwa matokeo ya tafiti za wataalamu wa afya tena na tena. Wanawauliza watu katika sehemu zenye malaria duniani, "Unafikiri nini kuhusu malaria?" Na hawasemi"Ni ugonjwa unaoua.Tunauogopa" Wanasema"Malaria ni tatizo la kawaida katika maisha" Haya ndiyo majibu niliyopata binafsi. Nilipowaambia ndugu zangu nchini India kwamba nilikuwa nikiandika kitabu kuhusu malaria waliniangalia kama Niliwaambia nilikuwa naandika kitabu kuhusu majipu au kitu fulani. kama,kwanini uandike kuhusu kitu kinachochosha. cha kawaida sana?unajua? Na ni muonekano rahisi lakini ni hatari. Mtoto nchini Malawi,kwa mfano, Anaweza akaugua malaria mara 12 kabla hajafika umri wa miaka miwili, lakini anaishi, ataendelea kupata malaria maisha yake yote, lakini uwezekano wa kufa kwa ugonjwa huo ni mdogo sana kwake. Kwa katika kuishi kwake, malaria ni kitu kinachokuja na kuondoka. Na hiyo ni kweli kwa malaria duniani. Malaria sehemu nyingi huja na kuondoka. Ni kwamba,kuna malaria sana kwamba sehemu hi ndogo ya matukio yanayopelekea kifo yanaongezeka kuwa katika namba kubwa. Kwa hiyi nadhani watu katika sehemu zenye malaria wanatakiwa kufikiri malaria katika njia ambayo sisi tunaoishi kwenye baridi tunafikiri kifua na mafua.Sawa? Mafua na kifua vina mzigo mkubwa sana katika jamii yetu na katika maisha yetu, lakini hatuchukui tahadhari zozote kwa sababu tunaona ni kawaida kupata mafua na kifua wakati wa nyakati za baridi.

8:31

Hii inaleta changamoto kubwa ya kitamaduni katika kupambana na malaria kwa sababu kama watu wanadhani ni kawaida kuwa na malaria, sasa kwa nini wanaenda kwa daktari kwenda kupimwa,kuandikiwa dawa wanazotakiwa tumia, kuchukua dawa zao, kuweka vifukuza mbu,kutumia chandarua? Hii inafanya kuendelea kuifuga malaria

8:56

Kwa hiyo chukua yote hayo. Tuna ugonjwa.Kisayansi umefumbika, una changamoto ya kiuchumi, na ndiyo watu ambao wanaosimama kufaidika wanaujali kwa hali ya chini sana. Na hiyo inaongeza tatizo kubwa sana katika yote, ambapo,kiukweli,ni tatizo la kisiasa. Unampata wapi kiongozi wa siasa kufanya chochote kwa tatizo kama hili? Na jibu ni kwamba,kihistoria,huwezi. Jamii nyingi zenye malaria kwa kipindi chote wameishi na ugonjwa. Kwa hiyo mashambulizi halisi kwenye malaria yametokea nje ya jamii zenye malaria, kutoka kwa watu ambao hawalazimishwi na hizi siasa zilizokufa. Lakini,nadhani,inaongeza aina nyingine za ugumu.

9:40

Shambulio la kwanza la kuangamiza malaria lilianza mwakani 1950. Ilikuwa ni mpangi uliosimamiwa na serikali. Na hizi juhudi zingekuwa na gharama sana kiuchumi. Walijua wanatakiwa kutumia zana na njia nafuu, wakawaza kutumia DDT. Walielewa changamoto ya kitamaduni. Kiukweli,mtazamao wao badala shupavu ulikuwa watu waliopo katika hatari ya malaria hawakutakiwa kufanya chochote kabisa. Kila kilitakiwa wafanyiwe. Lakini walididimiza sana changamoto ya kisayansi. Walikuwa na imani katika zana zao ambapo wakaacha kufanya tafiti za malaria. na wakati zana hizo zilipoanza kufeli, na maoni ya watu yakaanza kuziponda zana hizo, hawakauwa na wataalamu wa kisayansi kugundua ni lipi la kufanya. Kampeni hiyo ikaharibika,malaria ikarudi tena, lakini sasa ni mbaya sana kuliko mwanzoni kwa sababu ilifanyika katika sehemu ngumu kufikia katika njia ngumu za kudhibiti. Mmoja wa wafanyakazi wa WHO aliita kampeni yote hii "moja ya kosa kubwa lililowahi fanyika katika sekta ya afya"

10:44

Juhudi ya hivi karibuni ya kudhibiti malaria ilianza mwaka 1990. Iliongozwa na kupewa msaada wa kifedha kutoka katika jamii zisizo na malaria. Juhudi hizi sasa zinatambua kabisa changamoto ya kisayansi. Wanafanya tafiti nyingi sana za malaria. Na wanaelewa changamoto ya kiuchumi pia. Wanatumia vifaa nafuu sana na rahisi kutumia. Lakini sasa,nafikiri,njia panda ni changamoto ya ktamaduni. Juhudi za sasa ni chandarua. Kinawekewa dawa ya kuua mbu. Hiki kitu kimesambazwa kote katika sehemu zenye malaria kwa mamilioni. Na unapofikira kuhusu chandarua, ni aina ya kuingilia upasuaji. Unajua,haiongezi kitu chochote kwenye familia yenye malaria bali inasaidia kujikinga tu na malaria. Na tunawaambia watu watumie vyandarua kila usiku. Wanatakiwa walale kwenye vyandarua kila usiku. Na hivyo ndiyo njia pekee bora. Na wanatakiwa kufanya hivyo na hata kama chandarua kinazuia upepo mwanana, hata kama watatakiwa kuamka katikati ya usiku na kujipooza, hata kama watatakiwa kutoa vyombo vyao vyote ili kuweka chandarua, hata kama,unajua,wanaweza kuwa wanaishi kwenye nyumba za tembe za mviringo ambapo ni ngumu kuweka chandarua ya pembe nne. Sasa,hiyo haina maana kama unapambana na ugonjwa unaoua. Namaanisha,huu ni usumbufu mdogo. Lakini sivyo watu wenye malaria wanafikiri kuhusu malaria. Kwao,itakuwa tofauti kidogo.

12:09

Fikiri,kwa mfano,kundi la Wakenya wenye nia njema wakaja kwa sisi tuliopo katika nchi za baridi na wakasema, "Unajua,nyie watu mna mafua na kifua sana. Tumetangeneza hiki kifaa bora kabisa ambacho ni nafuu na rahisi kutumia, tutawapa bure. Inaitwa kinyago cha sura, na mnachohitaji ni kuvaa kila siku wakati wa kifua na mafua mnapoenda shule na mnapoenda kazini" Tutafanya hivyo?

12:35

Na nashangaa kama ni hivyo kwa watu katika sehemu zenye malaria wanafikiria hivi kwa hivyo vyandarua wanapovipokea? Tunajua kutoka katika tafiti kwamba asilimia 20 ya vyandarua ambazo zimesambazwa ndiyo zinazotumika. Na hiyo imepigia hesabu za juu sana, kwa sababu watu haohao wanaosambaza vyandarua walirudi na kuwauliza watumiaji, "mmetumia vyandarua nilivyowapa?" Ni sawa na shangazi yako Jane anakuuliza, "Umetumia chombo nilichokupa kwa ajili ya Krismas?" Kwa hiyo ni makadirio ya juu.

13:05

Lakini si kwamba tatizo suala la kupuuzia. Tunaweza kutoa elimu zaidi, tunaweza kuwashawishi hawa watu kutumia vyandarua. Na hicho ndicho kinachotokea sasa. Tunatumia muda na hela nyingi sana katika warsha na mafunzo na matamasha na michezo na vikao mashuleni, haya yote kushawishi watu kutumia vyandarua tulivyowapa. Na hiyo inaweza kufanya kazi. Lakini inatumia muda.Inagharimu pia. Inatumia rasilimali.Inatumia miundombinu. Inachukua vitu vyote nafuu, ambazo vyandarua havikutakiwa.

13:41

Kwa hiyo ni ngumu kushambulia malaria kutoka ndani ya jamii yenye malaria, Lakini inakuwa kidogo changamoto unapojaribu kushambulia malaria kutoka nje ya jamii hizo. Tunaweka vipaumbele vyetu katika jamii ya watu wenye malaria. Na hiki ndicho tulichofanya mwaka 1950. na hizo juhudi zilishindikana. Nitasema leo, tunaposambaza vifaa ambavyo tumetengeneza na ambavyo havina maana katika maiasha ya watu, tunajiweka katika hali ya kufanya kosa lingine.

14:11

Hiyo si kusema malaria kwamba hatuwezi kuishinda Malaria, kwa sababu nadhani tunaweza, lakini inakuwaje kama tukishambulia gonjwa hili kutokana na vipaumbele kwa watu walioishi nao? Chukua mfano wa Uingereza na Marekani. Tulikuwa na ugonjwa huo katika hizo nchi kwa mamia ya miaka, na tukaondokana nalo kabisa, sio kwamba tulishambulia malaria.Hapana. Tulishambulia barabara mbovu na nyumba mbovu na utoaji majitaka mbaya na ukosefu wa umeme na umasikini sehemu za vijijini. Tulishambulia maisha ya kuwa na malaria, na kwa kufanya hivyo,taratibu tukaondoa malaria. Sasa kushambulia maisha ya ki-malaria, hiki ni kitu-hivi ni vitu watu wanavyojala leo. Na kushambulia maisha ya kuishi na malaria, sio haraka,sio nafuu,sio rahisi, lakini nafikiri ni njia pekee ya kusonga mbele.

15:04

Asante sana

15:05

(Makofi)

Tumejua jinsi ya kutibu malaria tangu 1600,kwanini ugonjwa huu bado unaua maelfu ya mamia kila mwaka?ni zaidi ya tatizo la kitabibu,anasema mwandishi wa habari Sonia Shah.Mtazamo wa historia ya malaria unaweka wazi sababu tatu kwanini ni ngumu kutokomeza malaria

About the speaker
Sonia Shah · Science writer

Science historian Sonia Shah explores the surprisingly fascinating story behind an ancient scourge: malaria.

Science historian Sonia Shah explores the surprisingly fascinating story behind an ancient scourge: malaria.