Ngozi Okonjo-Iweala

Ngozi Okonjo-Iweala anazungumzia kufanya biashara Afrika

1,023,740 views • 20:13
Subtitles in 32 languages
Up next
Details
Discussion
Details About the talk
Transcript 32 languages
0:16

Asante sana Chris. Kila mtu aliyekuja hapa alisema kuwa anaogopa. Sijui kama na mimi ninaogopa, lakini hii ni mara yangu ya kwanza kuhutubia hadhara kama hii. Na sina teknolojia yeyote ya kisasa kwa ajili yenu ili muweze kuiangalia. Hakuna kielezopicha, kwa hiyo itabidi mnivumilie. (Kicheko).

0:37

Ninachotaka kufanya asubuhi hii ni kuwasimulia hadithi kadhaa na kuongelea kuhusu Afrika iliyo tofauti. Tayari asubuhi hii kulikuwa na madokezo kuhusu Afrika unayoyasikia kila mara: Afrika ya VVU/UKIMWI, Afrika ya malaria, Afrika ya umaskini, Afrika ya migongano, na Afrika ya maafa.

1:04

Ingawa kuna ukweli kwamba mambo hayo yanatokea, kuna Afrika ambayo hamuisikii sana. Na saa nyingine nashangazwa na kujiuliza kwanini. Hii ni Afrika ambayo inabadilika, ambayo Chris ameidokezea. Hii ni Afrika yenye fursa. Hii ni Afrika ambayo watu wanataka kuchukua hatua juu ya maisha na uwezo wao. Na hii ndio Afrika ambayo watu wanatafuta kuingia ubia kufanya hivyo. Na hili haswa ndilo ninalotaka kuzungumzia leo.

1:34

Ningependa kuanza kwa kuwaambia habari kuhusu mabadiliko hayo Afrika. Mnamo 15 Septemba 2005, Bwana Diepreye Alamieyeseigha, Gavana wa jimbo moja lenye utajiri wa mafuta huko Nigeria, alikamatwa na Polisi wa mji wa London alipokuwa matembizini mjini London. Alikamatwa kwasababu kulikuwa na hamisho la kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 ambazo zilienda katika akaunti hewa ambazo alikuwa akizimiliki yeye pamoja na familia yake. Kukamatwa kwake kuliwezekana kwasababu kulikuwa na ushirikiano baina ya Polisi wa mji wa London na Tume ya Uhalifu wa Kiuchumi na Fedha ya Nigeria — inayoongozwa na mtu wenye uwezo na ujasiri: Bwana Nuhu Ribadu. Alamieyeseigha alikamatwa mjini London. Kutokana na udhaifu, alifanikiwa kutoroka akiwa amevalia kama mwanamke na kukimbia kutoka London kurudi Nigeria ambako, kwa mujibu wa katiba, wale walio madarakani kama magavana, rais – kama ilivyo kwenye nchi nyingi — wana kinga na hawawezi kushtakiwa. Lakini nini kilitokea: watu walikasirishwa sana na tabia hii na iliwezekana kwa sheria za jimbo lake kumvua madaraka.

2:54

Leo, Alams – kama tumuitavyo kwa kifupi – yuko jela. Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wa Afrika hawako tayari tena kuvumilia rushwa kutoka kwa viongozi wao. Hii ni hadithi kuhusu ukweli kwamba watu wanataka rasilimali zao zidhibitiwe vizuri kwa manufaa yao, na sio kupelekwa sehemu ambako itawanufaisha mabwanyenye wachache. Kwa hiyo, unaposikia kuhusu Afrika ya rushwa — rushwa kila mara – Ninataka mfahamu kuwa watu na serikali wanajitahidi sana kupambana na tatizo hili katika baadhi ya nchi, na kwamba mafanikio yanaanza kuonekana.

3:36

Inamaana kuwa tatizo limekwisha? Jibu ni hapana. Bado kuna safari ndefu, lakini pia kuna nia. Mafanikio yanaandikwa juu ya mapigano ya jambo hili muhimu. Kwa hiyo mnaposikia kuhusu rushwa, msifikiri kwamba hakuna linalotendeka kuhusu hili — na kwamba hamuwezi kufanya kazi katika nchi yeyote Afrika kwasababu ya rushwa. Hiyo si kweli. Kuna nia ya kupambana na rushwa, na katika nchi nyingi, mapambano hayo yanaendelea na mafanikio yanaonekana. Katika nchi nyingine, kama yangu, ambako kumekuwa na historia ndefu ya kidikteta nchini Nigeria, mapambano bado yanaendelea, na bado tuna safari ndefu.

4:15

Ukweli wa mambo ni kwamba mapambano bado yanaendelea. Matokeo yanaonekana: tathmini huru ya Benki ya Dunia na mashirika mengine inaonyesha kuwa mwelekeo juu ya rushwa unapungua na utawala unarekebika. Utafiti uliofanywa na Tume ya Uchumi ya Afrika unaonyesha wazi mwelekeo mzuri wa utawala katika nchi 28 za Afrika.

4:41

Ngoja niseme kitu kimoja zaidi kabla sijamaliza kuzungumzia kuhusu utawala bora. Na ni kitu ambacho watu wanazungumzia kuhusu rushwa, rushwa. Kila mara wanapo zungumzia kuhusu hili mara moja unafikiria Afrika. Hiyo ndio picha: Nchi za Afrika. Lakini ngoja niseme hili: iwapo Alams alifanikiwa kuhamisha dola za kimarekani milioni 8 kwenye akaunti mjini London — kama watu wengine waliochukukua pesa wakikadiria kuwa kati ya bilioni 20 na 40 za pesa za nchi zinazoendelea ziko nje ya nchi katika nchi zilizoendelea – kama wanaweza kufanyi hivi, hiyo ni nini? Hiyo siyo rushwa? Katika nchi hii, kama ukipokea vitu vya wizi, haushitakiwi? Kwa hiyo tukiongelea kuhusu aina hii ya rushwa, hebu pia tufikirie kuhusu nini kinatokea katika upande mwingine wa dunia — ambako pesa hizo zinakwenda na nini kifanyike ili kuweza kuzuia hili. Kuna jambo ninalifanyia kazi kwa sasa, pamoja na Benki ya Dunia, kuhusu kurudisha rasilimali, tunajaribu tuwezalo kurudisha pesa ambazo zimepelekwa nje ya nchi — pesa za nchi zinazoendelea — ili ziweze kurudishwa. Kama tutaweza kurudisha dola bilioni 20 ambazo ziko nje, litakuwa jambo zuri sana kwa baadhi ya nchi hizi kuliko misaada yote ikiwekwa pamoja. (Makofi).

6:02

Kitu cha pili ninachotaka kuzungumzia ni nia ya mageuzi. Afrika, baada – wamechoka, tumechoka kuwa kitovu cha misaada kutoka kwa kila mtu. Tunashukuru, ila tunajua kuwa tunaweza kuchukua hatua juu ya uwezo wetu na kama tuna nia ya kufanya mabadiliko. Na kinachotokea katika nchi nyingi za Afrika sasa ni utambuzi kwamba hakuna anayeweza kufanya lolote ila sisi wenyewe. Ni lazima tufanye. Tunaweza kuwakaribisha washirika ambao wanaweza kutuunga mkono, lakini lazima tuanze wenyewe. Ni lazima turekebishe uchumi wetu, tubadilishe uongozi, tuwe na demokrasia zaidi, tuwe wazi kupokea mabadiliko na taarifa.

6:45

Na hiki ndicho tumeanza kukifanya katika mojawapo kati ya nchi kubwa kabisa katika bara, Nigeria. Hakika, kama hauko Nigeria, hauko Afrika. Ninataka kuwaambia kuwa. (Kicheko). Mmoja kati ya waafrika wanne walio kusini mwa jangwa la Sahara ni Mnigeria, na ina watu milioni 140 – watu wenye pilika — lakini watu wenye kuvutia. Hauwezi kuchoka. (Kicheko).

7:10

Tulichoanza kufanya ni kujua kwamba tunaweza kuchukua hatua na kujibadili wenyewe. Na kwa msaada wa kiongozi ambaye alikuwa na nia, kwa wakati ule, ya kufanya mabadiliko, tunaandaa mpango madhubuti wa mabadiliko ambao tumeuandika wenyewe. Si Shirika la Kimataifa la Fedha. Wala Benki ya Dunia, ambako nilifanya kazi kwa miaka 21 na kufikia cheo cha makamu wa rais. Hakuna mtu anaweza kukufanyia. Inabidi ufanye mwenyewe.

7:33

Tukaandaa mpango ambao kwanza, utafanya: kuiondoa serikali kwenye shughuli zisizo na manufaa — zisizoihusu — Serikali haitakiwi kufanya biashara ya uzalishaji na utoaji huduma kwasababu haina ufanisi na haina ujuzi. Kwa hiyo tuliamua kubinafsisha mashirika yetu mengi. (Makofi). Sisi — matokeo yake, tuliamua kuwa na soko huria. Unaweza kuamini kuwa kabla ya mabadiliko haya — ambayo yalianza mwishoni mwa mwaka 2003, wakati nilipoondoka Washington kwenda kushika nafasi ya Waziri wa Fedha — tulikuwa na kampuni ya simu ambayo iliweza kutoa huduma za simu za mezani 4,500 katika historia yake ya miaka 30? (Kicheko).

8:22

Kuwa na simu katika nchi yangu lilikuwa ni jambo la kifahari sana. Usingeweza kupata. Ilibidi uhonge. Ilibidi ufanye kila uwezalo ili kupata simu. Rais Obasanjo aliunga mkono na kuzindua kulegezwa kwa masharti katika sekta ya mawasiliano tumepanda kutoka simu 4,500 za mezani kufikia simu milioni 32 zenye GSM, na zinaongezeka. Soko la mawasiliano la Nigeria ni la pili kwa ukuaji duniani kote,♪ ikiwa imetanguliwa na China. Tunapata uwekezaji wa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka katika mawasiliano. Na hakuna mtu anayejua, isipokuwa kwa wajanja wachache. (Kicheko).

9:04

Wajanja wa kwanza kuja walikuwa ni kampuni ya MTN ya Afrika Kusini. Katika miaka mitatu niliyokuwa Waziri wa Fedha, wamepata wastani wa dola milioni 360 kwa mwaka. milioni 360 katika soko – katika nchi ambayo ni maskini, yenye wastani wa pato la taifa chini ya dola 500. Kwahiyo soko lipo hapo. Walilifanya hili siri, lakini baadae wengine nao walianza kujua. Wanageria wenyewe walianzisha makampuni ya mawasiliano ya simu zisizotumia waya na wengine kama watatu wane hivi wameingia. Lakini bado kuna soko kubwa sana, na watu hawajui kuhusu hili, au hawataki kujua. Kwa hiyo ubinafsishaji ni jambo mojawapo tulilofanya.

9:54

Kitu kingine tulichofanya ni kusimamia vizuri masuala yetu ya fedha. Kwasababu hakuna atakayekusaidia na kukuongoza iwapo hudhibiti fedha zako vizuri. Na Nigeria, ikiwa na sekta ya mafuta, ilikuwa na sifa ya rushwa na kutosimamia vizuri masuala ya fedha za umma. Je tulijaribu kufanya nini? Tulianzisha sheria ya fedha ambayo ilitenganisha bajeti yetu na bei ya mafuta. Zamani tulikuwa tumezoea kubajeti kutokana na kipato ambacho tulikipata kutokana na mafuta, kwasababu mafuta ndiyo sekta kuu ya mapato katika uchumi: asilimia 70 ya mapato yetu yanatokana na mafuta. Tulitenganisha hilo, na tulipofanya hivyo tulianza kubajeti kwa bei ambayo ilikuwa chini kidogo ya bei ya mafuta na kuhifadhi chochote cha ziada juu ya bei hiyo. Hatukuweza kujua kama tungeweza kufanikisha, ilikuwa ni utata sana.® Lakini kitu ambacho kilitokea haraka ilikuwa ni mabadiliko ambayo yalikuwepo kwa maendeleo yetu ya uchumi — ambapo, hata kama bei ya mafuta ingekuwa juu, tungekuwa haraka sana. Wakati zilipoanguka, tulianguka. Na tulikuwa tunashindwa kulipia chochote, hata mishahara, katika uchumi. Hii ilisawazisha. Tuliweza kuweka akiba, kabla sijaondoka, dola bilioni 27. Ambapo – hii ilienda kwenye hazina yetu — wakati nilipofika mwaka 2003, tulikuwa na dola billion 7 kwenye akiba. Na wakati naondoka, tulikuwa na karibu dola bilioni 30. Na tunavyoongea sasa, tuna dola bilioni 40 kwenye akiba hii ni kutokana na usimamizi mzuri wa fedha zetu. Hii inasaidia kutuliza uchumi wetu, kuufanya uwe imara.

11:37

Thamani ya fedha yetu ilikuwa ikibadilika kila mara kwa sasa ipo angalau imara na kusimamiwa, ili wafanyabiashara wawe na uhakika wa bei katika uchumi. Tuliweza kudhibiti mfumuko bei kutoka asilimia 28 mpaka karibu asilimia 11. Na pato letu la taifa liliongezeka kutoka wastani wa asilimia 2.3 kwa muongo uliopita mpaka kufikia asilimia 6.5 sasa. Kwa hiyo mabadiliko yote tuliyoweza kufanya yameweza kuonekana kwa vitendo ambavyo vinaweza kuonekana katika uchumi.

12:13

Na kitu cha muhimu zaidi, ni kwasababu tunataka kuondokana na mafuta na kupanua wigo zaidi – na kuna fursa nyingi sana katika nchi hii kubwa, kama ilivyo katika nchi nyingine za Afrika — kilichotia fora zaidi ni huu ukuaji haukutoka kwenye sekta mafuta pekee, bali sekta nyingine pia. Kilimo kilikuwa kwa wastani wa asilimi 8. Sekta ya mawasiliano ilikuwa, makazi na ujenzi, na ninaweza kuendelea zaidi na zaidi. Na hii ni kuwaonyesha kwamba uchumi wako unaporekebishika, fursa katika sekta nyingine zipo nyingi.

12:49

Tuna frusa katika kilimo, kama nilivyosema. Tuna fursa katika madini. Tuna madini mengi ambako hakuna mtu amewekeza katika utafutaji. Tumegundua kuwa bila kuwa na sera sahihi za kuwezesha, hilo halitawezekana. Sasa tuna sheria ya uchimbaji madini ambayo inalinganishwa na sheria nyingine bora duniani. Tuna fursa katika makazi na usimamizi wa majumba. Kulikuwa hakuna chochote katika nchi ya watu milioni 140 — hakuna maduka makubwa kama myajuavyo hapa. Hii inaweza kuwa fursa kwa mtu fulani ambayo ilitia chachu ya kufikiria kwa watu. Sasa tuna mazingira ambayo biashara katika maduka haya makubwa yanapata faida mara nne ya ilivyokadiriwa.

13:34

Kwa hiyo mambo makubwa kwenye ujenzi, mali isiyohamishika, Masoko ya rehani. Huduma za fedha tulikuwa na Benki 89. Nyingi hazifanyi biashara iliyokusudiwa. Tulizizatiti kutoka 89 kufikia Benki 25 kwa waongeze mtaji wao — gawio la mtaji. Ilikuwa kutoka dola milioni 25 mpaka dola milioni 150. Benki, Benki hizi sasa zimejizatiti na kuimarishwa mfumo wa Benki umevutia wamekezaji wengi kutoka nje. Benki ya Barclays kutoka Uingereza inaingiza milioni 500. Standard Chartered imeingiza milioni 140. Ninaweza kuendelea zaidi. Dola zaidi na zaidi, ndani ya mfumo.

14:17

Tunafanya hivyo hivyo kwenye sekta ya bima. Kwa hiyo kwenye huduma za fedha, kuna fursa kubwa zaidi. Kwenye utalii, katika nchi nyingi za Kiafrika, ni fursa kubwa. Na hii ndiyo sababu kubwa ya kuwa watu wengi wanaifahamu Afrika Mashariki kwa: wanyama pori, tembo na kadhalika. Lakini kusimimamia soko la utalii ili liweze kuwanufaisha watu ni muhimu sana.

14:41

Sasa ninachojaribu kusema ni nini? Najaribu kuwaambia kuna wimbi jipya katika bara. Wimbi la uwazi na demokrasia ambapo tangu mwaka 2000, zaidi ya theluthi mbili ya nchi za Afrika zimefanya uchaguzi wa kidemokrasia wa vyama vingi. Si zote zilikuwa kamilifu, au zitakuwa, lakini mwelekeo uko wazi. Ninajaribu kuwaelezea kwamba toka miaka mitatu iliyopita wastani wa ukuaji wa uchumi katika bara umeongezeka kutoka karibu asilimia 2.5 mpaka asilimia 5 kwa mwaka. Hii ni bora zaidi ya ufanisi wa nchi nyingi za OECD. Kwahiyo ni wazi kwamba mambo yanabadilika.

15:22

Migogoro imepungua barani; kutoka migogoro 12 kwa muongo uliopita, kufikia migogoro mitatu au minne, Mojawapo ya migogoro mibaya zaidi, kwa hakika, ni ule wa Darfur. Na kama ujuavyo, kuna athari kwa majirani, iwapo kuna jambo linatokea upande mmoja wa bara, inaonekana kama bara zima limeathirika. Lakini ni vema muelewe kwamba hili bara — ni bara lenye nchi nyingi na si nchi moja. Na iwapo tuna migogoro mitatu minne hivi, ina maana kuwa kuna fursa nyingi za kuwekeza katika uchumi ulio imara, unaokua na wenye kusisimua ambako kuna fursa nyingi sana. Ningependa kutoa dokezo moja kuhusu uwekezaji huu.

16:10

Namna nzuri ya kuisaidia Afrika sasa ni kuwasaidia waweze kusimama wenyewe. Na namna nzuri ya kufanya hivyo ni kusaidia kuleta ajira. Hakuna tatizo katika kupambana na malaria na kuwekeza pesa kwenye hilo na kuokoa maisha ya watoto. Sina maana hiyo. Hilo ni sawa. Lakini fikiria tofauti itakayokuwa kwenye familia: iwapo wazazi wanaweza kuwa na ajira na wakahakikisha watoto wao wanakwenda shule, kwamba wanaweza kununua dawa za kupambana na magonjwa wao wenyewe. Kama tunaweza kuwekeza kwenye maeneo ambayo nyinyi wenyewe mnapata faida wakati huo huo mkitengeneza ajira na kuwasaidia watu wasimame wenyewe, hii siyo fursa nzuri? Hii si ndiyo njia ya kufuata? Na nataka kusema jambo kuhusu watu bora zaidi wa kuwawekezea katika bara hili ni wanawake. (Makofi).

17:06

Nina CD hapa. Samahani sikusema kwa wakati muafaka. Lakini, ningependa mngekuwa mmeiangalia. Inasema, "Afrika: Iko wazi kwa Biashara." Na video hii imeshinda tuzo kama makala bora ya mwaka. Elewa kwamba mwanamke aliyetengeneza makala hii atakuwa Tanzania, ambako watakuwa na kongamano mwezi Juni. Lakini hii inakuonyesha kwamba Waafrika, na hususani wanawake wa Afrika, ambao pamoja na matatizo yote wameweza kuanzisha biashara, nyingine ni za kiwango cha kimataifa.

17:40

Mmoja kati ya wanawake katika video hii, Adenike Ogunlesi, anashona nguo za watoto kitu ambacho alianza kama kujifurahisha na ikakua na kuwa biashara. Akichanganya vitambaa vya Kiafrika ambavyo tunavyo, na vitambaa vingine kutoka sehemu nyingine. Na hivyo, atatengeneza suruali kwa kutumia vitambaa vizito, ikiwa imechanganywa na vitambaa vya kiafrika. Ni ubunifu mzuri sana. Amefikai hatua ambapo anapata zabuni kutoka Wal-Mart. (Kicheko). Kwa nguo 10,000 Kwa hiyo hii inawaonyesha kuwa tuna watu wenye uwezo wa kufanya mambo.

18:19

Wanawake wana juhudi, wako makini; wanachapa kazi. Naweza kuendelea kwa kutoa mifano: Beatrice Gakuba wa Rwanda, alifungua biashara ya maua na sasa anayasafirisha kwenye mnada wa udachi huko Amsterdam kila asubuhi, na ameajiri wanawake na wanaume takriban 200 kumsaidia kazi. Hata hivyo, wengi wao, wana kiu ya kupata mtaji wa kupanua biashara zao, kwasababu hakuna anayeamini nje ya nchi zetu tunaweza kufanya mambo ya maana. Hakuna mtu anayefikiria kwa mtazamo wa masoko. Hakuna anyefikiria kuna fursa Nimesimama hapa kuwaambia wale waliochelewa jahazi kwa sasa, watalikosa milele.

19:01

Kwa hiyo iwapo unataka kuwa Afrika, fikiria kuwekeza. Wafikirie akina Beatrice, wafikirie kina Adenike wa dunia hii. ambao wanafanya mambo makubwa ambayo yanawasogeza katika uchumi wa dunia, wakati huo huo wakihakikisha wanawake wenzao na wanaume wanapata ajira. na kwamba watoto katika familia hizo wanapata elimu kwa sababu wazazi wao wanapata kipato cha kuridhisha

19:29

Kwa hiyo nina wakaribisha kuja kutafuta fursa Mtakapo kwenda Tanzania, sikilizeni kwa makini, kwasababu nina hakika mtasikia kuhusu fursa mbalimbali zilizopo ili muweze kushiriki katika kufanya mambo mazuri kwa bara hili, kwa watu wake na kwenu wenyewe

19:52

Asanteni sana. (Makofi)

Tunajua mtazamo potofu kuhusu Afrika — njaa na magonjwa, vita na rushwa. Lakini, anasema Ngozi Okojo-Iweala, kuna mambo mengi yanayotokea katika nchi za Afrika ambayo hayazungumzwi: moja kati ya mabadiliko hayo, kukua kwa uchumi na fursa za kibiashara.

About the speaker
Ngozi Okonjo-Iweala · Economist

Ngozi Okonjo-Iweala is a respected global economist.

Ngozi Okonjo-Iweala is a respected global economist.