Kipi ambacho jalala lililopo Ghana linaweza kutufundisha kuhusu uvumbuzi
1,354,065 views |
DK Osseo-Asare |
TEDGlobal 2017
• August 2017
Sehemu iitwayo Agbogbloshie, jamii iliyopo Accra, Ghana, watu huenda kwenye jalala kuokota vifaa vibovu vya kielectroniki ili kupata malighafi. Bila mafunzo maalumu, wachimbaji hawa wa mjini hujifunza wenyewe jinsi gani vifaa hivi vinafanya kazi kwa kuvifungua na kuvifunga tena. Mshiriki wa TED DK Osseo-Asare anajiuliza: Kipi kitatokea kama tutaunganisha mafundi hawa waliojifundisha pamoja na wanafunzi na vijana wataalamu katika nyanja ya STEM(Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati)? Matokeo: jamii ya waundaji iliyo kubwa ambapo watu wanaungana pamoja na kuhamasika kutokana na kile wanachotaka kutengeneza. Jifunze zaidi ni namna gani sehemu hii ya uundaji inaongoza katika uchumi ulio na mzunguko katika ngazi ya chini.