David Steindl-Rast

Unataka kuwa na furaha? Kuwa mtu wa Shukrani

5,812,608 views • 14:30
Subtitles in 42 languages
Up next
Details
Discussion
Details About the talk
Transcript 42 languages
Translated by Nelson Simfukwe
Reviewed by Joachim Mangilima
0:11

Kuna kitu unafahamu kuhusu mimi,kitu cha binafsi sana, na kitu nafahamu kuhusu kila mmoja wenu na hicho ndiyo kitu kikuu kwa dhumuni lenu. Kuna kitu tunajua kuhusu kila mtu tunayekutana nae duniani, mtaani, hicho ndiyo kiini cha kila tunachofanya na chochote tunachokuwa pamoja nacho, ni kwamba wote tunataka kuwa na furaha. Katika hili,tupo pamoja. Tunavyofikiria furaha yetu. inatofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine, lakini ni vitu tulivyonavyo kwa pamoja, tunataka kuwa na furaha.

1:08

Sasa,mada yangu ni kuhusu kushukuru. Kuna uhusiano gani kati ya furaha na kushukuru? Watu wengi watasema,sawa,hiyo ni rahisi sana. Ukiwa na furaha,basi unashukuru. Lakini tazama tena. Ni kweli kwamba watu wenye furaha wana shukrani? Sote tunafahamu namba kiasi ya watu ambao wana kila kitu cha kuwafanya wawe na furaha, lakini hawa furaha, kwa sababu wanataka kitu kingine au wanataka kilekile lakini kwa mara nyingine. Na tunafahamu watu ambao ni fukara sana, ufukara ambao sisi hatutaki kuwa nao, lakini wamejawa na furaha mno. Wanamiminika furaha.Unashangaa. Kwanini?kwa sababu wanajua kushukuru. Kwa hiyo si furaha inayotufanya tuwe na shukrani. Ni shukrani inayotufanya tuwe na furaha. Kama unafikiri ni furaha inayotufanya tushukuru, tazama tena. Ni shukrani inayokufanya uwe na furaha.

2:25

Sasa,tunaweza kuuliza, nini maana ya shukrani? na inafanya kazi vipi? Nitarufaa katika uzoefu wako. Wote tunajua kutoka katika uzoefu inakuaje. Tunapata hali fulani ambayo ina thamani kwetu. Tunapata kitu chenye thamani. na kweli tunapata. Vitu hivi viwili vinatakiwa kuja pamoja. Inatakiwa kuwa na thamani, na ni zawadi halisi. Hujainunua.Hujaitolea jasho. Hujaifanyia biashara.Hujaifanyia kazi. Umepewa tu. na hivi vitu viwili vinapokuja pamoja, kile kilicho na thamani kwangu nagundua nimepewa bure, halafu shukrani muda huohuo inaamshwa katika moyo wangu, furaha muda huohuo pia inaamshwa katika moyo wangu. Hivyo ndivyo shukrani inavyotokea.

3:30

Sasa,ufunguo wa haya yote ni kwamba hatuwezi kukutana na hali hii mara moja. Hatuwezi kuwa na mazoea ya kushukuru tu. Tunaweza kuwa watu tunaoishi kwa shukrani. Kuishi ukiwa na shukrani,hicho ndo cha maana. Ni vipi tunaweza ishi tukiwa na shukrani? Kwa mazoea,kwa kujua kila wakati ni wakati tuliopewa,kama tusemavyo. Ni zawadi.Hujautolea jasho. Hujauleta kwa njia yoyote ile. Hauna njia ya kuhakikisha kwamba kutakuwa na wakati mwingine kwa ajili yako, na bado,hicho ni kitu muhimu sana ambacho tunaweza pewa, wakati huu,na nafasi zote ulizonazo. Kama tusingekuwa na wakati huu, tusingekuwa na nafasi ya kufanya lolote au kuzoea chochote, na wakati huu ni zawadi. Ni wakati tuliopewa,kama tusemavyo.

4:42

Sasa,tunasema zawadi ndani ya zawadi ni nafasi halisi. Unachoshukuru kwa hili ni nafasi, na sio kile ulichopewa, kwa sababu kama hicho kitu kingekuwa sehemu nyingine na hukuwa na nafasi ya kukifaidi, kufanya chochote nacho, usingeshukuru. Nafasi ni zawadi katika kila zawadi, na tunao huu msemo, nafasi huja mara moja tu. Sawa,fikiria tena. Kila wakati ni zawadi mpya,tena na tena, na kama utakosa nafasi ya wakati huu, wakati mwingine utakuja,na tena mwingine utakuja. Tunaweza pata nafasi tena au kukosa, na kama tutaipata nafasi, ni ufunguo wa furaha. Tunayo funguo kuu ya furaha yetu katika mikono yetu. wakati kwa wakati, tunaweza kuwa na shukrani kwa zawadi hii.

5:52

Ina maana kwamba tuwe na shukrani kwa kila kitu? Si hivyo. Hatuwezi kuwa na shukrani kwa vurugu,vita, kugandamizwa,kunyonywa na kuonewa. Katika hali ya utu,hatuwezi kuwa na shukrani kwa kupoteza marafiki,kwa kudanganywa, kwa kufiwa. Lakini sikusema tuwe na shukrani kwa kila kitu. Nimesema tuwe na shukrani kwa kila nyakati tunayopewa kwa nafasi, na hata tunapopingwa katika kitu ambacho ni kigumu sana, tunaweza ibuka katika hili na kuitikia nafasi tunayopewa. Sio mbaya kama inavyoonekana. Kiukweli,unapoiangalia na kuizoea, unakuta muda mwingi,tunachopewa ni nafasi ya kustarehe, na tunaikosa kwa sababu tunaharakisha maisha na hatuachi kuona nafasi.

7:00

Lakini wakati huo, tunapewa kitu kigumu, na hiki kitu kigumu kinapokuja, ni changamoto katika kuifanikisha ile nafasi, na tunaweza fanikiwa kwa kujifunza kitu ambacho wakati mwingine kinaumiza. kujifunza uvumilivu,mfano. Tunaambiwa kwamba njia ya amani sio ya harakaharaka, lakini ni ya kukimbia kama marathon. Inahitaji uvumilivu.Hiyo ni ngumu. Inaweza kuwa kusimama kwa maoni yako, kusimama kwa ajili ya ushawishi wako. Hiyo ni nafasi tunayopewa. Kujifunza,kuumia,kusimama, nafasi hizi zote tunapewa, lakini ni nafasi, na wote wanaozitumia nafasi hizo ndiyo tunaowathamini. Wanafanya kitu katika maisha. Na wale wanaofeli wanapata nafasi nyingine. Siku zote tunapata nafasi nyingine. Huo ndo uzuri wa maisha.

8:09

Kwa hiyo ni jinsi gani tunatafuta namna katika kuendelea na kukuza hili? Jinsi gani kila mmoja wetu atatafuta njia ya kuishi kwa shukrani, sio mara moja tu kuwa na shukrani, lakini wakati hadi wakati. Tunaweza kufanyaje? Ni rahisi sana. Ni rahisi sana,kama tulivyoambiwa wakati tukiwa watoto tulijifunza kukatiza mitaani. Simama.Angalia.Nenda. Hivyo tu. Lakini ni mara ngapi tunasimama? Tunaharakisha katika maisha.Hatuachi. Tunakosa nafasi kwa sababu hatuachi. Tunatakiwa kuacha.Tunatakiwa kunyamaza. Na tunatakiwa kutengeneza alama za tahadhari katika maisha yetu.

9:02

Nilipokuwa Afrika miaka michache iliyopita nikarudi tena, Niligundua maji. Nilipokuwa Afrika,sikuwa na maji ya kunywa. Muda wote nilipofungua bomba, Nilifarijika. Muda wote nilipowasha taa, Nilishukuru.Nilifurahishwa sana. Lakini baada ya muda,vyote vilipotea. Kwa hiyo nikaweka stika ndogo katika sehemu ya kuwashia taa na katika bomba la maji, na kila wakati nikifungua,maji. Kwa hiyo achilia katika fikra zako. Unaweza tafuta chochote kilicho bora kwako, lakini unahitaji alama za tahadhari katika maisha yako. Na unaposimama. kinachofata ni kuangalia. Unaangalia.Unafungua machi yako. Unafungua masikio.Unafungua pua. Unafungua milango yote ya fahamu kwa huu utajiri mzuri tuliopewa. Hauna mwisho, na hivyo maisha yalivyo, kufurahia,kufurahi kile tulichopewa.

10:05

Na baada ya hapo tunaweza fungua mioyo yetu, kwa ajili ya nafasi, kwa nafasi ya kutusaidia, kuwafanya wengine wawe na furaha,kwa sababu hamna kinachotufanya tuwe na furaha sana kama wote tukiwa na furaha. Na wakati tunafungua mioyo kwa ajili ya nafasi tupewazo, nafasi zinatualika kufanya kitu fulani, na ni cha tatu. Simama,angalia,halafu nenda,na fanya kitu kweli. Na tunachoweza kufanya ni chochote ambacho maisha yamekupa kwa wakati huo. Mara nyingi ni nafasi ya kufurahi, lakini wakati mwingine ni kitu kigumu.

10:50

Lakini vyovyote ilivyo,kama tutaichukua nafasi hii, tukaenda nayo,sisi ni wabunifu, hao ni watu wabunifu, na hiyo simama,angalia,nenda, ni mbegu bora sana inayoweza badilisha dunia. Kwa sababu tunahitaji,tupo katika kipindi cha sasa katikati ya mabadiliko ya dhamira, na utashangaa kama uki Siku zote nahamaki ninaposikia ni mara ngapi hili neno"shukrani" na "kushukuru" yanapokuja. Kila unapoyakuta, ndege ya kushukuru,mgahawa wa shukrani, Mvinyo wenye shukrani. Ndiyo,nimewahi ona karatasi ya chooni alama yake ya biashara inaitwa Nashukuru((Vicheko) Kuna wimbi la shukrani kwa sababu watu wanaanza kugundua ni muhimu kiasi gani na jinsi gani itabadili dunia. Inaweza badili dunia yetu na katika njia muhimu sana, kwa sababu kama una shukrani,hauna uoga, na kama hauna uoga,hauna vurugu. Kama una shukrani,unaenenda katika hali ya kutosha na sio katika hali ya upungufu, haupo tayari kugawana. Kama una shukrani,unafurahia tofauti kati ya watu, na heshima yako kwa kila mtu, na hiyo inabadili piramidi la nguvu ambalo tunaishi sasa.

12:22

Na haileti usawa, lakini inaleta heshima sawa, na hicho ni kitu muhimu. Dunia ya baadaye itakuwa mtandao, sio piramidi,ambalo limegeuzwa juu chini Mabadiliko ninayoongelea sio mabadiliko ya vurugu, na mabadiliko sana ambayo yanabadilisha maana halisi ya mapinduzi, kwa sababu mapinduzi ya kawaida ni yale ambayo piramidi linageuzwa juu chini na wale walio chini wanakuwa juu na wa juu nao chini yameahafanyika huko nyuma Tunachohitaji ni mtandao wa vikundi vidogo, vikundi vidogo na vidogo vinavyotambuana, vinavyokutana pamoja, na hiyo ni dunia nzuri sana.

13:13

Dunia nzuri yenye watu wenye furaha sana. Watu wenye shukrani ni watu wenye furaha tele, na watu wenye furaha tele, wanavyozidi kuwa watu wengi wenye furaha na hivyo tutakuwa na dunia yenye watu wenye furaha zaidi. Tuna mtandao wa maisha ya kushukuru, na ina uyoga. Na hatuwezi kuelewa kwanini ina uyoga. Tuna nafasi ya watu kuwasha mshumaa wanaposhukuru kwa jambo fulani. Na kuna mishumaa milioni 15 inayowashwa katika muongo mmoja. Watu wanaanza kutambua dunia ya shukrani ni dunia yenye furaha, na wote tuna nafasi kwa njia rahisi ya simama,angalia,nenda, kubadilisha dunia, kuifanya sehemu ya furaha. Na hilo ndo ninalotumaini kwetu, na kama hili linachangia kidogo kwa kukufanya uhitaji kufanya hichohicho, simama,angalia,nenda.

14:15

Asante.

14:16

(Makofi)

Kitu kimoja ambacho binadamu wote tunacho pamoja ni kuwa na furaha,anasema kaka David Steindl-Rast,mtawa na mwanafunzi wa imani.Na furaha,anasema,inazaliwa kutoka katika shukrani.Somo linalohamasisha katika kwenda polepole,kuangalia unapokwenda,na kwa hayo yote,kuwa na shukrani.

About the speaker
David Steindl-Rast · Monk

Brother David Steindl-Rast, a Benedictine monk, meditates and writes on "the gentle power" of gratefulness.

Brother David Steindl-Rast, a Benedictine monk, meditates and writes on "the gentle power" of gratefulness.