Return to the talk Watch the talk

Subtitles and Transcript

Select language

Translated by Joachim Mangilima
Reviewed by Nelson Simfukwe

0:11 Kuna njia nyingi ambazo watu wanaotuzunguka wanaweza kuboresha maisha yetu Hatuonani na jirani zetu kwa hiyo maarifa mengi yanashindwa kusambaa pamoja na kwamba wote tunashiriki sehemu zile zile za jamii yote

0:24 Kwa hiyo miaka michache iliyopita, nimejaribu kutafuta njia za kushirikiana zaidi na majirani zangu katika maeneo ya jamii yote Kwa kutumia vifaa rahisi kama stika ,karatasi nyembamba na chaki Mipango hii ilitokana na maswali niliyokuwa nayo kama Ni kiasi gani majirani zangu wanalipa kwa ajili ya nyumba zao? (Vicheko) Je ni jinsi gani tunaweza kuazimishana vitu vingi zaidi bila kugonga katika milango wakati usio mzuri? Je tunawezaje kushirikishana kumbukumbu zetu zaidi za majengo yetu yaliyotelekezwa na kuyaelewa zaidi mazingira yetu Ni vipi tunaweza kushirikishana matumaini yetu zaidi. kuhusu maduka yasiyo na watu, ili jamii zetu ziendane na mahitahi yetu na ndoto zetu?

1:05 Sasa naishi New Orleans, Ninaipenda New Orleans Nafsi yangu inaburudishwa na miti mikubwa ya mwalo inayowafunika wapenzi,walevi na watu wanaowaza mambo makubwa kwa mamia ya miaka, na nauamini mji ambao wakati wote una njia kwa ajili ya muziki Nahisi kama kila wakati ambapo mtu atakuwa anakoroma, New Orleans kuna gwaride.(Vicheko) Mji huu una baadhi ya majengo ambayo ni mazuri sana katika dunia,lakini pia una namba kubwa ya majengo yaliyotelekezwa katika nchi ya Marekani

1:34 Ninaishi karibu na nyumba hii, na nilifikiri ni jinsi gani ninavyoweza kuifanya kuwa sehemu nzuri kwa ajili mtaa wangu, na pia niliwaza kuhusu kitu kingine ambacho kilibadilisha maisha yangu milele

1:47 Mwaka 2009,nilifiwa na mtu ambaye nilimpenda sana, Jina lake ni Joan,na alikuwa ni mama yangu Kifo chake kilikuwa cha ghafla bila kutarajiwa Niliwaza sana kuhusu kifo na hii ilinifanya nijae moyo wa shukrani kwa muda nilio nao na ilinisaidia kuangalia vizuri vitu vyenye maana katika maisha yangu kwa sasa. Lakini napata shida kudumu katika hali hii katika maisha yangu ya kila siku. Nahisi ni rahisi kusongwa na matukio ya kila siku, na kusahau mambo ya maana hasa kwako.

2:35 Kwa hiyo kwa msaada wa marafiki wa zamani na wapya, Niligeuza upande wa nyumba hii iliyotelekezwa na kuwa ubao mkubwa sanana kuuwekea karatasi nyembamba na sentensi ambayo ilitakiwa ijazwe ikisema "Kabla sijafa,nataka Kwa hiyo kila aliyepita aangeweza kuchukua chaki, kutafakari maisha yake,na kutoa mawazo yake katika eneo la wazi

2:57 sikujua niwaze nini kuhusu jaribio hili lakini mpaka siku iliyofuata, ukuta wote ulijaa na uliendelea kukua. na ningependa nitawashirikisha vitu vichache ambavyo watu waliandika katika ubao huu.

3:12 "Kabla ya kufa,ningependa nishitakiwe kwa uharamia."(Vicheko) ."Kabla ya kufa,nataka kusafiri kuufuata mstari wa kimataifa wa tarehe" "Kabla ya kufa,nataka niimbe kwa ajili ya mamilioni." "Kabla ya kufa,nataka nipande mti." "Kabla ya kufa,nataka niishe bila kutegemea umeme." "Kabla ya kufa,nataka nimkumbatie tena kwa mara nyingine." "Kabla ya kufa,nataka niwe askari wa farasi." "Kabla ya kufa,nataka kuwa peke yangu."

4:04 Kwa hiyo sehemu hii iliyotelekezwa ikageuka kuwa sehememu ya matengenezo, matumaini na maono ya watu ilinifanya nicheke, nilie na kwa njia hii walinifariji katika wakati wangu mgumu. Ni kwa ajili ya kujua kuwa hauko peke yako. Ni kwa ajili ya majirani zetu kwa njia mpya na za kupendeza ni kwa aajili ya kuwa na nafasi ya kutafakari na kuwaza yale unayoyapenda kuwa nayo na kukumbuka ni nini hasa ambacho ni cha muhimu kwa wengi wetu kadiri tunavyokua na kubadilika

4:32 nilifanya hivi mwaka jana, na nikaanza kupokea mamia ya jumbe kutoka kwa watu ambao walitaka kutengeneza mbao na kuta kama hii katika jamii zao, kwa hiyo washirika wangu na mimi tukatengeneza boksi la vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya kazi hii na kwa sasa kuta kama hii zimetengenezwa sehemu mbalimbali duniani, Ikiwemo Kazakhstan, Afrika ya Kusini, Australia, Argentina na zaidi ya hapo Pamoja,tumeonyesha jinsi sehemu za wazi zinavyoweza kuwa na uwezo mkubwa kama tutapewa nafasi ya kuongea na kushirikishana.

5:08 Vitu vya thamani zaidi tulivyo navyo ni muda na mahusiano yetu na watu wengine Katika wakati huu ambao kuna mambo mengi ya kututoa katika mambo muhimu, Ni muhimu sana kutafuta njia za kudumu katika mambo muhimu na kukumbuka kuwa maisha ni mafupi na mepesi Mara nyingi tunavunjwa moyo kuongelea kuhusu kifo au kuwaza kuhusu kifo,lakini nimetambua kuwa kujiandaa na kifo ni moja kati ya vitu vya kukujenga sana kufikiri kuhusu kifo , kunayafafanua maisha yako.

5:40 Maeneo ya wazi na jamii yote yanaweza yakaonyesha ni kitu gani muhimu kwetu kwa mtu mmoja mmoja na kama jamii, na tukiwa na njia nyingi za kushirikishana matumaini, hofu na hadithi zetu, watu wanaotuzunguka sio tu wanaweza kutusaidia kufanya maeneo haya kuwa mazuri, lakini wakaishi vizuri pia. Asante.(Makofi)

5:59 (Makofi) Asante.(Makofi) (Makofi)