Mirejesho ya bidhaa tunazonunua mtandaoni inakwenda wapi?
1,916,651 views |
Aparna Mehta |
TED@UPS
• July 2018
Huwa unaagiza nguo mtandaoni katika ukubwa na rangi mbalimbali, ili tu kujaribisha na kisha kurudisha ambazo hazikufai? Aparna Mehta alikuwa akifanya hivi nyakati zote, mpaka ilipofika siku alipojiuliza: Ni wapi ambapo nguo zinazorudishwa huenda? Katika hotuba yake ambayo inafumbua macho, anatufunulia dunia isiyoonekana ya "mrejesho wa bure wa bidhaa za mtandaoni" -- ambapo, badala ya kurudi katika makabati, hupelekwa katika jalala takribani paundi bilioni kila mwaka -- na anatueleza mpango wa kusaidia kukomesha ukuaji wa janga hili la kimazingira.