Return to the talk Watch the talk

Subtitles and Transcript

Select language

Translated by Hector Mongi
Reviewed by Joachim Mangilima

0:11 Mwaka jana nilionyesha hizi kurasa mbili ili kuthibitisha kuwa barafu inayofunika arctic, ambayo kwa zaidi ya miaka milioni tatu iliyopita imekuwa na ukubwa unaopungua kidogo ya ule wa majimbo 48, imepungua kwa asilimia 40. Lakini hii inapunguza msisitizo wa tatizo hili mahsusi kwa sababu haionyeshi unene wa barafu. Mfuniko wa barafu wa arctic ni, kwa matazamo, Mapigo ya moyo wa mfumo wa tabia nchi wa dunia. Inatanuka wakati wa masika na kusinyaa wakati wa kiangazi. Kurasa inayofuata nawaonesha (barafu) itatoweka kwa kasi zaidi kuliko ilivyotokea miaka 25 iliyopita. Barafu ya kudumu imewekewa alama nyekundu. Kama mnavyoona, inatanuka kuelekea rangi ya bluu iliyokolea. Hiyo ni barafu ya mwaka wakati wa masika. Na inasinyaa wakati wa kiangazi. Kilichoitwa barafu ya kudumu, katika umri wa miaka mitano, mnaona imekuwa kama damu, ikitiririka kutoka mwilini hapa. Ndani ya miaka 25 imetoweka kutoka hii, hadi hii.

1:05 Hili ni tatizo kwa kuwa kuongezeka kwa joto, kunapasha ardhi iliyoganda kuzunguka bahari ya arctic ambayo ina kiasi kikubwa cha ukaa ulioganda ambao, unapoyeyuka, unabadilishwa na wadudu wadogo kuwa methini. Ukilinganisha na jumla ya uchafuzi wa anga wenye kuleta ongezeko la joto duniani, Kiasi hiki chaweza`kuwa mara mbili endapo tutavuka ncha hii hatari. Tayari katika maziwa ya kina kifupi yaliyoko Alaska methini inatoka majini kama mapovu yenye nguvu. Profesa Katey Walter kutoka Chuo Kikuu cha Alaska alienda pamoja na timu nyingine kwenye ziwa jingine fupi wakati wa masika iliyopita. Whoa! Yuko sawa. Swali ni iwapo tutakuwa.

1:52 Na sababu moja ni, hili joto kuu linaloshuka likipasha joto Greenland kutoka kaskazini. Huu ni mto unaoyeyuka mwaka mzima. Lakini kiasi cha ujazo ni kikubwa kuliko wakati wote. Huu ni mto Kangerlussuaq kusini magharibi mwa Greenland. Kama unataka kujua jinsi kina cha bahari kinavyoongezeka kutokana na kuyeyuka kwa ardhi-barafu hapa ndipo huingilia baharini. Mitiririko hii inaongezeka kwa kasi sana. Pale Antarctica, mwisho mwingine wa sayari, kuna mlundikano mkubwa zaidi wa barafu katika sayari hii. Mwezi uliopita wanasayansi waliripoti bara nzima lina barafu katika mizania hasi. Na Antarctica magharibi ambayo imezuka ghafla juu ya baadhi ya visiwa ndani ya bahari, Ni mahsusi kwa kuyeyuka haraka. Hiyo si sawa na futi 20 za usawa wa bahari, kama ilivyo Greenland.

2:33 Himalaya, ina mkusanyiko wa barafu wa tatu kwa ukubwa, Juu yake unaona maziwa mapya, ambayo miaka michache iliyopita yalikuwa barafu. Asilimia 40 ya watu wote duniani wanapata nusu ya maji ya kunywa kutokana na kuyeyuka kunakotoa mtiririko huo. Katika Andes, hii barafu ni chanzo cha maji ya kunywa kwa jiji hili. Mitiririko imeongezeka. Lakini kadiri yanavyotoweka, vivyo hivyo na maji ya kunywa Huko California asilimia 40 ya mlundikano ya barafu wa Sierra umepungua. Hili linaathiri akiba ya maji. Na tabiri, kama mlivyosoma, ni makini.

3:01 Huku kukauka kwa dunia kumepelekea Ongezeko kubwa la mioto. Na maafa duniani kote yamekuwa yakiongezeka kwa kiwango kisicho cha kawaida na kwa kasi ya kutisha. Mara nne zaidi katika miaka 30 iliyopita kama ilivyo kwa miaka 75 ya karibuni. Huu ni mpangilio usio endelevu kabisa. Kama ukiangalia katika muktadha wa historia unaweza kuona hii inafanya nini.

3:28 Katika miaka mitano iliyopita Tumeongeza tani milioni 70 za hewa ya ukaa kila saa 24 — tani milioni 25 kila siku kwenda baharini. Angalia kwa makini eneo la mashariki mwa Pacific, kutoka Amerika, likitanuka kuelekea magharibi na upande wowote wa bara dogo la India, ambako hewa ya oksijeni katika bahari inaisha kwa kasi. Sababu moja kubwa ya ongezeko la joto duniani sambamba na ukataji hovyo wa miti, ambao ni asilimia 20, ni nishati itokanayo na visukuku Mafuta ni tatizo, na makaa ya wawe ni tatizo kubwa kuliko yote. Marekani ni moja ya nchi mbili kubwa zinazotoa gesi joto, sambamba na China. Na pendekezo limekuwa kujenga viwanda zaidi vya makaa ya mawe.

4:05 Lakini tulikuwa tunaanza kuona badiliko. Hapa ni mpango mmoja uliovunjwa miaka michache iliyopita Kukiwa na mapendekezo mbadala ya kijani. (Makofi) Hata hivyo kuna vita ya kisiasa nchini mwetu. Na viwanda vya makaa ya mawe na viwanda vya mafuta vilitumia dola robo bilioni katika mwaka wa kalenda uliopita kutangaza makaa safi ya mawe, ambayo ni utatanishi. Picha hiyo ilinikumbusha kitu (Kicheko) Karibia na Krismas, nyumbani kwangu Tennessee, galoni bilioni za majimaji ya makaa ya mawe zilivuja. Huenda mliiona kwenye habari. Hiki, nchini kote, ni kijito cha pili kwa ukubwa cha uchafu katika Marekani. Hii ilitokea karibu na Krismas. Moja ya matangazo kutoka kiwanda cha makaa ya mawe karibia Krismas lilikuwa hili,

4:48 Bila bashasha Kaa-jiwe-mtu ni mchangamfu, akiishi kwa furaha. Anapatikana kwa wingi hapa Marekani, Na anasaidia uchumi wetu kukua. Bila bashasha kaa–jiwe-mtu anakuwa safi kila siku, gharama yake ni ndogo na anapendwa, na watumishi wanabakiza malipo yao.

5:03 Hiki ni chanzo cha kiasi kikubwa cha makaa ya mawe katika Virginia Magharibi Mchimbaji mkubwa kuliko wote ni mkuu wa kampuni ya makaa ya mawe ya Massey

5:12 Ngoja niwe wazi kuhusu hiyo. Al Gore, Nancy Pelosi, Harry Reid, hawajui wanalozungumzia.

5:18 Kwa hiyo Muungano wa Kulinda Tabia Nchi umezindua kampeni mbili. Hii ni mojawapo, sehemu ya mojawapo.

5:25 Pale COALergy tunaona mabadiliko ya tabia nchi kama tishio kubwa kwa biashara zetu. Ndio maana tumelifanya lengo letu la msingi kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika juhudi za kutangaza kuweza kuuweka wazi na kwa ujumla wake uweki kuhusu makaa ya mawe. Ukweli ni kuwa, makaa ya mawe sio uchafu. Tunadhani ni safi – ina harufu nzuri, pia. Hivyo msijali kuhusu mabadiliko ya tabia nchi. Tuachie sisi. (Kicheko)

5:50 Makaa safi ya mawe, mmesikia mengi kuyahusu. Hivyo hebu tutalii nyenzo yetu mahiri ya makaa safi ya mawe. Yashangaza! Mashine ni aina ya kelele. Lakini hiyo ni sauti ya teknolojia ya makaa safi ya mawe. Na wakati kuchoma makaa ya mawe ni moja ya sababu kuu za ongezeko la joto duniani, teknolojia ya kipekee ya makaa safi ya mawe mnayoona hapa inabadilisha kila kitu. Angalia kwa kirefu, hii ni teknolojia ya kisasa ya makaa safi ya mawe.

6:18 Mwisho mbadala chanya Unaoana na changamoto zetu za kiuchumi na changamoto zetu za usalama wa taifa.

6:24 Marekani ipo katika mzozo, uchumi, Usalama wa taifa, mzozo wa tabia nchi. Utando unaziunganisha zote, mazoea yetu ya nishati zitokanazo na ukaa, kama makaa ya mawe chafu na mafuta ya kigeni. Lakini sasa kuna suluhisho mpya thabiti la kututoa katika vurugu hili. Kuipa nguvu mpya Marekani kwa kuwa na umeme safi kwa asilimia 100, ndani ya miaka 10. Mpango wa kuirejesha Marekani kazini, unatufanya tuwe salama, na unasaidia kusimamisha ongezeko la joto duniani. Mwisho, suluhisho lililo kubwa vya kutosha kusuluhisha matatizo yetu. Kuipa nguvu mpya Marekani. Tafuta zaidi.

6:53 Hii ni ya mwisho.

7:02 Inahusu kuipa nguvu mpya Marekani. Moja ya njia za haraka kupunguza utegemezi wetu kwenye nishati chafu ya kizamani inayoua sayari yetu. Mustakabali wetu upo hapa. Upepo, jua, nishati mpya ya gridi. Uwekezaji mpya unaotengeneza ajira mpya zenye malipo makubwa. Ipe nguvu mpya Marekani. Ni wakati wa kupata usahihi.

7:25 Kuna methali ya kale ya Kiafrika isemayo, "Kama unataka kwenda haraka, nenda mwenyewe. Kama unataka kwenda mbali, nenda pamoja." Tunataka kwenda mbali, kwa haraka. Asanteni sana. (Makofi)