Takriban miaka 10 iliyopita, nilianza kazi ya kufundisha maendeleo ya ulimwengu kwa wanafunzi wa Kiswidishi wa shahada ya kwanza. Hii ilikuwa baada ya takriban miaka 20 ya kufanya kazi pamoja na taasisi mbalimbali za Afrika nikitafiti kuhusu njaa katika Afrika, kwa hiyo nilikuwa natarajiwa niwe najua zaidi kuhusu dunia. Na nilianzia kwenye chuo chetu cha utabibu, Taasisi ya Karolinska, kozi ya shahada ya kwanza iliyoitwa Afya ya Ulimwengu. Lakini ukipata fursa hiyo, unapata mshawasha kidogo. Nilifikiri wanafunzi hawa kuja kwetu ni lazima wana maksi za juu unazoweza kupata kwenye mfumo wa vyuo vya Sweden -- kwahiyo labda wanajua kila kitu kuhusu nitakachowafundisha. Kwa hiyo niliwapa mtihani mara tu walipokuja. Na moja wapo kati ya maswali ambayo nilijifunza mengi ni hili hapa: "Ni nchi gani kati ya hizi tano ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto kati ya jozi hizi tano?"
Na niliziweka pamoja, ili katika kila kundi la nchi, moja ina kiwango kikubwa cha vifo vya watoto zaidi ya nyingine. Na hii inamaanisha kwamba kuna tofauti kubwa sana kuliko uhakika wa takwimu. Sitawapa mtihani hapa, lakini ni Uturuki, ambayo ina kiwango kikubwa pale, Poland, Urusi, Pakistani na Afrika Kusini. Na haya ndiyo majibu ya wanafunzi wa Kiswidishi. Nilifanya hivyo na nilipata kiwango cha imani, ambacho kilikuwa kidogo, na nilifurahi, kwa hakika: 1.8 ya jibu sahihi kati ya matano inawezekana. Hii ina maana kwamba kulikuwa kuna nafasi ya Profesa wa afya ya ulimwengu -- (Kicheko) na kwa kozi yangu.
Lakini usiku mmoja, wakati nilipokuwa natayarisha ripoti Niligundua uvumbuzi wangu. Nimeonyesha kuwa wanafunzi Waswidishi wenye alama za juu wanajua kidogo sana kuhusu takwimu za ulimwengu kuliko hata sokwe. (Kicheko) Kwasababu sokwe wangepata nusu iwapo ningewapa ndizi mbili zenye Sri Lanka na Uturuki. Wangekuwa sahihi kwa nusu yake.
Lakini wanafunzi hawapo huko. Tatizo langu halikuwa kutokujua kwao: ilikuwa ni mawazo waliyojijengea.
Pia nilifanya utafiti kinyume na maadili kwa maprofesa wa taasisi ya Karolinska (Kicheko) -- ambao wanatoa tuzo ya Nobel katika utabibu, na wao wako sawa tu na sokwe. (Kicheko) Hapa ndipo nilipogundua kwamba kuna haja ya kuwasiliana, kwasababu ya takwimu za kinachotokea duniani na afya ya mtoto katika kila nchi inajulikana.
Tulitengeneza hii programu ya kompyuta ambayo inayoonyesha kama hivi: kila kiputo hapa ni nchi. Hii nchi hapa ni China. Hii ni India. Ukubwa wa kiputo ni idadi ya watu, na katika mhimili huu nimeweka kiwango cha uzazi. Kwasababu wanafunzi wangu, walichosema wakati walipoangalia dunia, na nilipowauliza, "Nini mnafikiri kuhusu dunia?" Naam, kwanza niligundua kuwa kitabu cha kiada kilikuwa Tintin, angalau. (Kicheko) Na walisema, "Dunia bado ni 'sisi' na 'wao.' Na sisi ni dunia ya Magharibi na wao ni Dunia ya Tatu." "Na una maana gani kwa kusema dunia ya magharibi?" Niliuliza. "Naam, haya ni maisha marefu na familia ndogo, na dunia ya tatu ni maisha mafupi na familia kubwa."
Kwa hiyo hii ndio ninayoweza kuonyesha hapa. Niliweka kiwango cha uzazi hapa: idadi ya watoto kwa mwanamke, moja, mbili, tatu, nne, mpaka watoto nane kwa mwanamke mmoja. Tuna takwimu nzuri sana toka mwaka 1962 -- 1960 kuhusu -- ukubwa wa familia katika nchi zote. Kiwango cha makosa ni kidogo sana. Hapa naweka umri wa kuishi wakati wa kuzaliwa, kuanzia miaka 30 katika nchi nyingine mpaka karibu miaka 70. Na mwaka 1962 kulikuwa na kundi kubwa la nchi hapa, ambazo zilikuwa nchi zenye viwanda, na walikuwa na familia ndogo na maisha marefu. Na hizi zilikuwa nchi zinazoendelea: walikuwa na familia kubwa na walikuwa na maisha mafupi. Sasa nini kimetokea toka mwaka 1962? Tunataka kuona mabadiliko. Je wanafunzi wako sahihi? Bado ni aina mbili za nchi? Au hizi nchi zilizoendelea zina familia ndogo na wanaishi hapa? Au wana maisha marefu na wanaishi hapo juu?
Hebu tuone. Tulisimamisha dunia wakati ule. Hizi zote ni takwimu za Umoja wa Mataifa ambazo zinapatikana. Hebu tuone. Unaweza kuona kule? Ni China kule, ikiendelea dhidi ya afya bora hapa, inaboreka kule. Nchi zote za kijani za Amerika ya Kusini zimeanza kuelekea kuwa na familia ndogo. Hizi za njano hapa ni nchi za Kiarabu, na wana familia kubwa, lakini wao -- hawana maisha marefu, lakini si familia kubwa. Waafrika ni kijani hapa chini. Bado wamebaki hapa. Hii ni India. Indonesia inaenda kwa kasi sana. (Kicheko) Na miaka ya 80 hapa, kuna Bangladesh bado iko miongoni mwa nchi za Afrika kule. Lakini sasa, Bangladesh -- ni miujiza iliyotokea miaka ya 80: Maimamu walianza kuhamasisha uzazi wa mpango. Walisogea juu kwenye ile kona. Na katika miaka ya 90, tulikuwa na janga la Ukimwi ambalo lilishusha umri wa kuishi wa nchi za Afrika na nyingine zote zilipanda kwenye ile kona, ambako tuna maisha marefu na familia ndogo, na tuna ulimwengu mpya kabisa. (Makofi)
Ngoja nifananishe kati ya Marekani na Vietnam. 1964: Marekani ilikuwa na familia ndogo na maisha marefu; Vietnam ilikuwa na familia kubwa na maisha mafupi. Na hiki ndicho kilichotokea: takwimu wakati wa vita zilionyesha kuwa pamoja na vifo vyote, kulikuwa kuna mabadiliko katika umri wa kuishi. Mwisho wa mwaka, uzazi wa mpango ulianza Vietnam na waliamua kuwa na familia ndogo. Na Marekani pale juu wanakuwa na maisha marefu, wanabaki na ukubwa wa familia. Na miaka ya 80 sasa, waliacha mpango wa kikomunisti na wakaingia kwenye uchumi wa soko huria, na inaenda haraka hata zaidi ya maisha ya jamii. Na leo, Vietnam ina umri wa kuishi na ukubwa wa familia sawa hapa Vietnam, 2003, kama ilivyokuwa Marekani, 1974, mwishoni mwa vita. Nafikiri sote -- kama hatutaangalia vielelezo -- tutapuuza mabadiliko makubwa huko Asia, ambayo yalikuwa mabadiliko ya kijamii kabla hatujaona mabadiliko ya kiuchumi.
Hebu tuendelee kwingine hapa ambako tunaweza kuonyesha mgawanyo wa kipato duniani. Hii ni mgao wa kipato cha watu. Dola moja, dola 10 au dola 100 kwa siku. Hakuna pengo tena kati ya matajiri na maskini. Hii ni hali ya kufikirika Kuna kituta kidogo hapa. Lakini kuna watu kila sehemu. Na tukiangalia kipato kinapoishia -- kipato hicho -- hii ni asilimia 100 ya kipato cha dunia kwa mwaka. Na asilimia 20 ya matajiri wakubwa kabisa, wanachukua karibu asilimia 74. Na asilimia 20 ya masikini zaidi, wanachukua karibu asilimia mbili. Na hii inaonyesha kwamba dhana ya nchi zinazoendelea ni ya mashaka. Tunafikiria kuhusu misaada, kama watu hawa wanatoa misaada kwa watu wale pale. Lakini katikati, tuna idadi kubwa ya watu duniani, wenye asilimia 24 ya kipato.
Tuliyasikia haya kwa namna nyingine. Na hawa ni akina nani? Nchi mbalimbali ziko wapi? Naweza kukuonyesha Afrika. Hii ni Afrika. Asilimia 10 ya idadi ya watu duniani, wengi wao wako kwenye umaskini. Hii ni OECD. Nchi tajiri. Nchi za kundi la Umoja wa Mataifa. Na wapo huku upande huu. Kuna mwingiliano kati ya Afrika na OECD Hii hapa ni Amerika Kusini. Ni kila kitu katika dunia hii, kuanzia maskini zaidi mpaka matajiri, huko Amerika Kusini. Zaidi ya hayo, tunaweza kuiweka Ulaya Mashariki, Asia Mashariki, na Asia Kusini. Na ingekuwaje iwapo tungerejea nyuma, mpaka mwaka 1970? Wakati huo kulikuwa na nundu kubwa zaidi. Na waliokuwa kwenye umaskini mkubwa zaidi ni Waasia. Tatizo la dunia lilikuwa umaskini huko Asia. Na sasa kama nitaicha dunia isogee mbele, utaona kwamba wakati idadi ya watu inaongezeka, kuna mamia ya milioni huko Asia wanajikwamua kutoka umaskini na wengine wanaingia katika umaskini, na hii ndiyo hali tuliyonayo leo hii. Na makadirio mazuri kutoka Benki ya Dunia, ni kwamba haya yatatokea, na hatutakuwa na dunia iliyogawanyika. Tutakuwa na watu wengi katikati.
Naam, hiki ni kipimo cha logarithm, lakini dhana yetu ya uchumi ni kukua kwa asilimia. Tunaiangalia kama ni uwezekano wa kuongezeka kwa asilimia. Kama nitabadili hii, na kuchukua GDP kwa taifa badala ya kipato cha familia, na ninabadili hivi takwimu moja moja kwenye takwimu za kanda za GDP, na ninazileta kanda hapa chini, ukubwa wa kiputo bado ni idadi ya watu. Na una OECD pale, na una Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara hapo, na tunatoa nchi za Kiarabu pale, zinatoka Afrika na Asia, na tunaziweka tofauti, na tunaweza kuukuza muhimili huu, na ninaipa vipimo vipya hapa, kwa kuongeza thamani ya ustawi wa jamii pale, uwezekano wa kusalimika mtoto. Sasa nimeweka pesa pale kwenye mhimili, na nina uwezekano wa watoto kusalimika pale. Katika baadhi ya nchi, asilimia 99.7 ya watoto wanaishi mpaka miaka mitano; wengine, mika 70 tu. Na hapa inaonekana kuna pengo kati ya OECD, Amerika Kusini, Ulaya Mashariki, Asia Mashariki, Nchi za kiarabu, Asia Kusini na Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Uwiano baina ya maisha ya watoto na pesa ni wa karibu sana.
Lakini hebu niigawanye Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara. Afya iko hapa na afya bora iko kule. Ninaweza kwenda hapa na kuigawa Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara katika nchi tofauti. Na ikipasuka, ukubwa wa puto la nchi ni sawa na idadi ya watu. Hapa chini ni Siera Leone. Mauritus iko pale juu. Mauritius ilikuwa nchi ya kwanza kuondokana na vikwazo vya biashara, na waliweza kuuza sukari yao. Waliweza kuuza nguo kwa taratibu sawa na watu wa Ulaya na Amerika Kaskazini.
Kuna tofauti kubwa sana ndani ya Afrika. Na Ghana iko hapa katikati. Huko Siera Leone, misaada ya kibinadamu. Hapa Uganda, misaada ya maendeleo. Hapa, muda wa kuwekeza, kule, unaweza kwenda kwa mapumziko. Ni tofauti kubwa sana katika Afrika ambayo mara nyingi tunaitambua -- kuwa iko sawa kwa kila kitu. Naweza kuigawa Asia Kusini hapa. India ni kiputo kikubwa cha katikati. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya Afghanistani na Sri Lanka. Naweza kugawa nchi za Kiarabu. Wakoje? Hali ya hewa sawa, utamaduni sawa, dini sawa. Tofauti kubwa. Hata kati ya majirani. Yemen, vita vya wao kwa wao. Umoja wa Falme za Kiarabu, pesa ya kutosha ni sawa na ikatumiwa vizuri. Sio kama tunavyofikiria. Na hii inajumuisha watoto wa raia wa kigeni ambao wapo nchini. Takwimu ni bora zaidi ya unavyofikiria. Watu wengi wanasema takwimu ni mbaya. Kuna nafasi ya mashaka, lakini tunaweza kuona tofauti hapa: Cambodia, Singapore. Tofauti ni kubwa zaidi ya udhaifu wa takwimu. Ulaya Mashariki: Uchumi wa Kisovieti muda mrefu, lakini waliweza kujikwamua baada ya miaka kumi kwa utofauti sana. Na kuna Amerika Kusini. Leo, hatuna haja ya kwenda Cuba kutafuta nchi yenye afya bora Amerika Kusini. Chile itakuwa na idadi ndogo ya vifo vya watoto zaidi ya Cuba miaka michache ijayo kuanzia sasa. Na hapa tuna nchi zenye kipato kikubwa katika OECD.
Na hapa tunapata mwelekeo wote wa ulimwengu, ambao ni karibu ni sawa na hali hii. Na tukiiangalia, inavyoonekana -- dunia, mwaka 1960, inaanza kusogea. 1960. Huyu ni Mao Tse-tung. Alileta afya China. Halafu akafariki. Halafu akaja Deng Xiaoping na akaleta pesa kwa China, na kuwapandisha chati tena. Na tumeona jinsi nchi zinavyosogea katika mwenendo tofauti kama hivi, kwa hiyo inakuwa vigumu kupata mfano wa nchi ambayo inaonyesha mwelekeo wa ulimwengu. Ningependa kuwarudisha nyuma mpaka karibu na mwaka 1960. Ningependa kulinganisha Korea Kusini ambayo ni hii hapa, na Brazil, ambayo ni hii hapa. Kibandiko kimetoka hapa. Na ningependa kufananisha Uganda, ambayo iko kule. Na ninaweza kuileta mbele, kama hivi. Na unaweza kuona jinsi Korea Kusini wanavyosonga mbele kwa kasi sana, wakati Brazil inakwenda polepole.
Na kama tukirudi nyuma tena, hapa, na tukiweka alama juu yao, kama hivi, unaweza kuona tena kuwa kasi ya maendeleo ni tofauti sana, na nchi zinasogea sana au kidogo katika kiwango sawa na kukua kwa pesa na afya, lakini inaonekana unaweza kusogea haraka sana iwapo una afya kwanza kuliko ukiwa na pesa kwanza. na kuonyesha hii, unaweza kuweka Umoja wa Falme za Kiarabu. Walitokea hapa, nchi ya madini. Walivuna mafuta yote, walipata pesa zote, lakini afya haiwezi kununuliwa dukani. Inabidi uwekeze kwenye afya. Inabidi uwapeleke watoto shule. Inabidi kuwafunza wafanyakazi wa afya. Inabidi kuwaelimisha watu. Na Sheikh Sayed alifanya hivyo kwa namna nzuri. Pamoja na kuanguka kwa bei ya mafuta, aliipandisha nchi yake hapa juu. Kwa hiyo tumepata muelekeo wa ulimwengu, ambapo nchi zote zinatabia ya kutumia pesa zao vizuri zaidi ya walivyokuwa wakitumia huko nyuma. Naam, hivi ndivyo, zaidi au pungufu kidogo, ukiangalia wastani wa takwimu za nchi. Ziko kama hivi.
Sasa hii ni hatari, kutumia wastani wa takwimu, kwasababu kuna tofauti kubwa kati ya nchi. Kwa hiyo nikienda kuangalia hapa, tunaona kuwa Uganda ya leo ni mahali ambapo Korea ya Kusnini ilikuwa mwaka 1960. Na kama nikiigawa Uganda, kuna tofauti ndani ya Uganda. Hii ni moja ya tano ya takwimu ndani ya Uganda. Asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Uganda wako pale. Masikini zaidi wako hapa chini. Iwapo nikiigawa Afrika Kusini, iko kama hivi. Na iwapo nikiangalia Niger, ambako kulikuwa na ukame mbaya sana, mwishoni, iko kama hivi. Asilimia 20 ya masikini zaidi huko Niger wako hapa, na asilimia 20 ya matajiri zaidi wa Afrika Kusini wako kule, na bado tunatabia ya kuzungumzia kuhusu utatuzi upi unafaa kwa matatizo ya Afrika. Kila kitu kilichopo hapa duniani kinapatikana Afrika. Na hamuwezi kuongelea upatikanaji wa dawa za VVU [madawa] kwa moja ya tano hapa juu kwa mkakati sawa kama hapa chini. Maendeleo ya ulimwengu ni lazima yawekwe kwa makundi tofauti, na si lazima kuwa nayo katika ngazi ya kanda. Ni lazima tuingie ndani zaidi. Tumetambua kuwa wanafunzi wanapatwa na mshawasha wakiweza kutumia hii.
Na wapanga sera na sekta binafsi zingependa kuona namna gani dunia inabadilika. Sasa, kwanini hii haitokei? Kwanini hatutumii takwimu tulizonazo? Tuna takwimu katika Umoja wa Mataifa, na katika taasisi za takwimu za nchi na katika vyuo vikuu na mashirika yasiyo ya kiserikali. Kwasababu takwimu zimefichwa kwenye masijala. Na umma uko pale, na mtandao wa Intaneti uko, lakini bado hatujautumia ipasavyo.
Taarifa zote tunazoziona zikibadilika duniani hazihusishi takwimu zinazogharimiwa na umma. Kuna baadhi ya kurasa za tovuti mfano hii, kama ujuavyo, lakini zinachukua kutoka kwenye masijala ya takwimu, lakini watu wanaziwekea bei, funguo za siri na takwimu za kuchosha. (Kicheko). (Makofi).
Na hii haitatusaidia. Sasa nini kinatakiwa? Tuna masijala za takwimu. Si masijala mpya ya takwimu unayoihitaji. Tuna vifaa vizuri vya ubunifu, na vingi vinaongezewa hapa. Kwa hiyo tulianzisha shirika lisilo la kibiashara ambalo tukaliita -- kuunganisha takwimu kwa ubunifu -- tunaiita Gapminder, kutoka London chini ya ardhi, ambako wanakuonya, "angalia upenyo" Kwa hiyo tulifikiri Gapminder ilikuwa ni sahihi. Na tulianza kuandika programu ya kompyuta ambayo ingeweza kuunganisha takwimu kama hivi. Na haikuwa vigumu sana. Iliwachukua watu wengine miaka kadhaa, na tumetengeneza vielelezo. Unaweza kuchukua seti ya takwimu na kuiweka hapa. Tunakomboa takwimu za Umoja wa Mataifa, mashirika machache ya Umoja wa Mataifa.
Nchi nyingine zinakubali takwimu zao ziwe wazi duniani, lakini tunachohitaji zaidi ni, kwa hakika, namna ya kuzichambua. Programu ya kutafuta ambayo itakuwezesha kunakili takwimu katika muundo wa kutafutika na kuiweka wazi duniani. Na nini tunasikia tuzungukapo? Nimefanya anthopolojia katika sehemu kubwa za takwimu. Kila mtu anasema, "Haiwezekani. Hii haiwezi kufanyika. Taarifa zetu ni za ovyoovyo kwa ndani, na kwahiyo haziwezi kupangiliwa zitafutike kama nyingine zinavyoweza kutafutwa. Hatuwezi kutoa takwimu bure kwa wanafunzi, bure kwa wajasiliamali wa dunia." Lakini hivi ndivyo tungependa tuone, au sio? Takwimu zilizogharimiwa na umma zipo hapa chini. Na tungependa maua yaote nje kwenye mtandao. Na jambo la muhimu zaidi ni kuzipangilia ili ziweze kutafutika, na watu waweze kuzitumia vifaa tofauti vya ubunifu kueleleza pale. Nina habari nzuri kwenu. Nina habari nzuri kwamba, Mkuu wa Kitengo cha Takwimu cha Umoja wa Mataifa, hasemi haiwezekani. Anasema, "Hatuwezi kufanya." (Kicheko) Huyu ni mtu mwenye akili, eeeh? (Kicheko)
Kwa hiyo tunaona mambo mengi yakitokea kwenye takwimu katika miaka ijayo. Tutaweza kuangalia mgawanyo wa kipato katika namna mpya kabisa. Huu ni mgao wa kipato huko China, 1970, mgao wa kipato wa Marekani, 1970. Karibu hakuna mwingiliano, karibu hakuna mwingiliano. Na nini kimetokea? Kilichotokea ni hiki: China inakua, haiko sawa tena, na inatokea hapa, ikiingalia Marekani. Kama vile mzuka, au sio, eeeh? (Kicheko)
Inatisha. Lakini nadhani ni muhimu sana kuwa na taarifa hizi. Tunahitaji sana kuziona. Badala ya kuangalia hii, ningependa kumalizia kwa kuwaonyesha watumiaji wa mtandao kwa kila 1,000. Katika programu hii ya kompyuta, tunaweza kupata karibu alama 500 kutoka katika nchi zote kwa urahisi. Inachukua muda kubadilika kwa hii, lakini katika mihimili, unaweza kupata alama yeyote utakayopenda kupata. Na kitu kizuri itakuwa ni kuziweka masijala za takwimu bure, kuweza kuzifanya ziweze kutafutika, na kuzipata kwa kubonyeza kwa nukta moja kwenye mfumo wa michoro majira ya nukta, ambapo utazielewa kwa urahisi. Naam, wanatakwimu hawazipendi, kwasababu wanasema kuwa hii haitaonyesha hali halisi; inabidi tuwe na mbinu za kuchambua takwimu. Lakini hii inajenga nadharia.
Ninamalizia sasa na dunia. Pale, mtandao wa intaneti unakuja. Idadi ya wanaotumia mtandao inaongezeka kama hivi. Hii ni GDP per capita Na ni teknolojia mpya inayokuja, lakini cha kushangaza, ni namna ambavyo inashabihiana na hali ya uchumi wa nchi. Ndio maana kompyuta ya dola 100 itakuwa ya muhimu sana. Lakini ni muelekeo mzuri. Ni kama vile dunia inakuwa bapa. Au sio? Nchi hizi zinanyanyuka zaidi ya uchumi na itakuwa ni ya kufurahisha kufuatilia hii kwa miaka ijayo, na kama ambavyo ningependa muweze kufanya kwa kutumia takwimu zilizogharamiwa na umma. Asanteni sana. (Makofi)
You can share this video by copying this HTML to your clipboard and pasting into your blog or web page. This video will play with subtitles.
You either have JavaScript turned off or have an old version of the Adobe Flash Player. To view this rating widget you
need to get the latest Flash player.
If your browser allows only "trusted sites" to execute Javascript, you should add the "googleapis.com" domain to your whitelist to allow our Flash detection to work properly.
Got an idea, question, or debate inspired by this talk? Start a TED Conversation.
Hujapata kuona takwimu zikielelezwa namna hii. Kwa ufundi na umahiri wa kuhadhiri, gwiji wa takwimu Hans Rosling anachambua mtazamo potofu uitwao "nchi zinazoendelea."
In Hans Rosling’s hands, data sings. Global trends in health and economics come to vivid life. And the big picture of global development—with some surprisingly good news—snaps into sharp focus. Full bio »
18:57 Posted: Jun 2007
Views 2,161,521 | Comments 221
16:51 Posted: May 2008
Views 430,015 | Comments 118
17:56 Posted: Aug 2010
Views 1,347,980 | Comments 248
Just follow the guidelines outlined under our Creative Commons license.
This comment will be attributed to . Not ? Sign Out.