nina furaha kubwa kuwa kati ya mwanga unasumbua sana macho yangu na unaakisiwa katika miwani yangu Ni furaha na heshima kwangu kuwa kati ya watu wabunifu na wenye ufahamu wa hali ya juu nimewasikiliza wazungumzaji watatu waliopita na jaribu kufikiri nini kilichotokea? kila kitu nilichopanga kuzungumza wameshakiongea, na inaonekana sasa ni kama sina chochote cha kuongea
lakini kuna msemo katika jamii yangu kuwa kama jani likidondoka kutoka mtini bila kusema chochote basi jani hilo ni changa kwa hiyo kwa kuwa si mchanga nami nina umri mkubwa sana bado nitaongea kitu
tunaandaa mkutano huu katika wakati ambao umejaa fursa nyingi kwa kuwa mkutano mwingine unafanyika katika mji wa Berlin(Ujerumani) na huu ni mkutano wa G8 mkutano huu wa G8, unapendekeza kuwa ufumbuzi wa matatizo ya Afrika ni ongezeko maradufu la misaada, hatua ambayo inafanana na mpango wa Marshall bahati mbaya ni kuwa mimi siamini katika mpango huu wa Marshall kwanza, kwa sababu faida za mpango huu wa Marshall zimeongezwa chumvi. waliopokea msaada mkubwa kupitia mpango huu walikuwa ni ujerumani na ufaransa, na msaada huu ulikuwa ni asilimia 2.5 tu ya pato lao la taifa(GDP) kwa wastani nchi yoyote Afrika inapokea misaada kutoka nje kufikia kiwango cha asilimia 13, 15 ya pato la taifa, huu ni uhamishaji wa rasilimali za kiuchumi mkubwa sana kutoka nchi tajiri kwenda nchi maskini
lakini kuna vitu viwili ambavyo tunahitaji kuviunganisha navyo ni jinsi vyombo vya habari vinavyoionyesha Afrika katika nchi za magharibi na madhara yake kwa kuonyesha majonzi, matatizo na ukosefu wa matumaini vyombo vya habari vinaonyesha ukweli kuhusu Afrika,na si vinginevyo zaidi ya ukweli. lakini vyombo vya habari havielezi ukweli wote. kwa sababu huzuni,vita vya wenyewe kwa wenyewe na njaa ingawa ni sehemu ya ukweli kuhusu Afrika lakini sio ukweli pekee na pili ni sehemu ndogo sana ya ukweli
bara la Afrika lina mataifa 53 lakini tuna vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi sita tu, hii inamaanisha kwamba vyombo vya habari vinaonyesha nchi sita tu Afrika ina fursa nyingi ambazo hazijatolewa katika mzunguko wa matatizo na kukosa msaada ambao vyombo vya habari vya magharibi vinaonyesha kwa watazamaji wao lakini madhara ya hali hii ni kuwa inaleta hali ya huruma inaleta hali ya huruma na kusaidia kwa hiyo mwonekano kwa nchi za magharibi kuhusu matatizo ya kiuchumi ya afrika unakuwa mbaya mwonekano huu mbaya ni zao la mawazo kuwa afrika ni sehemu ya matatizo tuifanyie nini?tupeleke chakula kwa wenye njaa tupeleke madawa kwa wagonjwa tupeleke majeshi ya kulinda amani kuwalinda wanaokabiliwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe. na katika hali hii afrika imenyang'anywa kujitegemea yenyewe
nataka kusema kuwa ni muhimu kuelewa kuwa afrika ina udhaifu wa msingi lakini pia ina fursa nyingi na uwezo mkubwa tunahitaji kubadilisha fikra kuhusu changamoto zinazoikabili Afrika kutoka changamoto za matatizo matatizo yanayoitwa upunguzaji wa umaskini kuwa changamoto ya matumaini tunahitaji kuonyesha kuwa ni changamoto ya matumaini changamoto inayowakabili wote wanaoipenda Afrika siyo changamoto ya kupunguza umaskini bali ni changamoto ya kutengeneza mafanikio
ni mpaka tutakapobadilisha vitu hivi viwili ukisema Waafrika ni maskini na wanahitahitaji kupunguza umaskini utakuwa na ushirika wa kimataifa wenye nia ya kusaidia ukiingia afrika na nini? dawa kwa ajili ya maskini,msaada wa chakula kwa ajili ya wenye njaa na walinda amani kwa wale wanaokabiliwa na vita za wenyewe kwa wenyewe na mwisho vitu hivi vyote havisaidii chochote kwa sababu unatibu dalili na sio chanzo cha msingi cha matatizo ya Afrika kumpeleka mtu shule na kumpatia dawa mabibi na mabwana, hakutengenezi mafanikio kwa ajili yao mafanikio yanatokana na kipato,kipato kinachokuja kutokana na kupata fursa ya biashara yenye faida au ajira inayolipa vizuri
kwa hiyo tunaapoanza kuongelea kutengeneza mafanikio katika Afrika changamoto yetu ya pili itakuwa ni, ni kina nani ambao ni mawakala wa utengenezaji wa mafanikio katika jamii yoyote ni wajasiriamali ..[haileweki] .... alituambia kuwa siku zote asilimia 4 ya watu,lakini asilimia 16 ni waigaji lakini pia wanafanikiwa katika ujasiriamali kwa hiyo tuwekeze pesa zetu wapi sasa? tunahitaji kuwekeza pesa zetu pale ambapo itazaa wezesha uwekezeji binafsi Afrika,uwekezaji kutoka ndani na nje wezesha taasisi za utafiti, kwa sababu maarifa ni sehemu muhimu ya utengenezaji wa mafanikio
lakini ni nini jumuiya ya misaada ya kimataifa inafanya afrika leo? wanatupa kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya huduma za msingi za afya, elimu na misaada ya chakula. bara lote limegeuzwa kuwa ni, sehemu ya matatizo inayohitaji msaada mabibi na mabwana,kuna yeyote anayeweza kuniambia jirani,rafiki,ndugu unayemjua ambaye alikuwa tajiri kwa kupokea misaada? kwa kushika bakuli la kuombea? kuna mtu yeyote kati yenu aliye na mtu wa aina hiyo? kuna yeyote anayejua nchi iliyoendelea kwa sababu ya huruma na ukarimu wa nchi nyingine? kwa kuwa sioni mkono wowote inaonekana ninachokiongea kuwa ni sahihi
Andrew Mwenda: naona bono anasema anaijua nchi hiyo. ni nchi gani hiyo?
asante sana. lakini naomba nikwambie kuwa wasaidizi kutoka nje watakachokupa ni fursa tu uwezo wa kuitumia na kuigeuza kuwa faida unategemea na uwezo ulionao afrika imepata fursa nyingi nyingi kati ya hizo hazijatusaidia sana. kwa nini? kwa sababu tumekosa uwezo kutoka ndani na sera zitakazowezesha kufaidika na mahusiano yetu ya nje.nitatoa mfano
chini ya makubaliano ya Cotonou zamani yakijulikana kama makubaliano ya Lome nchi za afrika zimepewa nafasi na bara la ulaya ya kusafirisha bidhaa bila ushuru katika soko lao Nchi yangu mwenyewe,Uganda imepewa kuuza kiasi cha tani 50 000 za sukari kwenda katika soko la ulaya mpaka sasa hatujauza hata kilo moja tunaagiza tani 50 000 za sukari kutoka brazili na Cuba pili,upande wa nyama katika makubaliano haya nchi za afrika zinazozalisha nyama zimepewa kiasi cha kuuza bila ushuru katika soko la ulaya hakuna nchi yoyote ikiwamo botswana,nchi iliyofanikiwa sana afrika ambayo imefanikiwa kufikia kiwango hicho
kwa hiyo nataka kusema kuwa msingi wa afrika kushindwa kushirikiana kikamilifu na nchi nyingine duniani katika mahusiano ya kiuchumi ni kwa sababu ya uwezo mbovu kitaasisi na kisera njia zozote za utatuzi zinahitaji msaada kuanzishwa kwa taasisi zinazotengeneza mafanikio taasisi zinazoongeza uzalishaji tunaanzaje kufanya hivyo na kwa nini misaada si njia nzuri? misaada si njia nzuri,unajua ni kwa nini? ni kwa sababu serikali zote duniani zinahitaji pesa ili zidumu pesa inahitajika kwa ajili ya kufanya vitu kama kuhakikisha usalama. unahitaji kulipa wanajeshi na polisi kulinda usalama. na kwa sababu serikali zetu nyingi ni za kidikteta wanahitaji jeshi kunyanyasa wapinzani na pili unahitaji kulipa washirika wako wa kisiasa kwa nini watu waisaidie serikali yao? kwa sababu inawapa kazi yenye malipo mazuri au,katika nchi nyingi za africa,nafasi zisizo rasmi za kujinufaisha na rushwa
ukweli ni kwamba hakuna serikali duniani ukiondoa chache kama ile ya Idi Amin ambazo zitategemea nguvu katika kutawala nchi nyingi katika [haileweki],zinahitaji uhalali kujihalalisha, serikali mara nyingi inaleta vitu kama elimu ya msingi huduma za afya,barabara, hospitali na vituo vya afya kama kusimama kwa serikali kiuchumi kunategemea kuingiza pesa kutoka kwa watu wake serikali kama hiyo inaendeshwa na maslahi binafsi ikitawala kwa kutoa amri itakaa na wanaoingiza fedha kuongea nao kuhusu sera na taasisi ambazo ni muhimu kwao kwa ajili ya kukuza biashara zao ili iweze kukusanya kodi zaidi kutoka kwao tatizo la bara la afrika na mashirika ya misaada ni kwamba imeharibu mfumo wa kujitegemea unaozikumba serikali za Afrika inatafuta mapato ya maana sio katika uchumi wa ndani bali kutoka kwa wafadhili
baada ya kukaa na wajasiriamali wa Uganda wafanyabiashara wa Ghana,au viongozi wa viwanda wa afrika ya kusini serikali zetu zinaona ni bora kuongea na IMF na benki ya dunia hata kama utakuwa na madaktari wa falsafa kumi hauwezi kumshinda Bill Gates kuhusu ufahamu wa biashara ya kompyuta kwa nini?kwa sababu maarifa yanayohitajika ili uelewe jinsi ya kukuza biashara yanahitaji uwasikilize watu walio katika sekta binafsi
serikali za afrika kwa hiyo zimepewa nafasi na jamii ya kimataifa kujiondoa katika kujenga mipango endelevu na wananchi wao na kufanya majadiliano yasiyoisha na IMF na benki ya dunia na baada ya hapo ni IMF na benki ya dunia ambao wanawaeleza kile wananchi wao wanachihitaji katika hali hiyo watu wa afrika wanaachwa pembeni katika utengenezaji na utekelezaji wa sera katika nchi zetu tunakuwa hatuna mchango, kwa kuwa amlipaye mpiga filimbi ndiye anayechagua wimbo IMF, Benki ya dunia na muunganiko wa watoa misaada wametunyang'anya haki zetu sisi kama raia kwa hiyo ambacho serikali zetu inafanya kwa kuwa zinategemea misaada ni kuwasikiliza wafadhili kuliko wananchi wao wenyewe
lakini nataka niweke angalizo katika maelezo yangu na angalizo hili ni kuwa si kila msaada ni mbaya baadhi ya misaada inaweza ikawa imejenga hospitali na kulisha wenye njaa inaweza ikawa imejenga barabara na hiyo barabara inaweza ikawa imefanya kazi nzuri Kosa la jamii ya misaada ya kimataifa ni kuchagua mafanikio haya machache na kuingiza mabillioni kwa matrillioni ya Dola na baadaye kuyatangaza dunia nzima wakisahau mazingira mengine tofauti katika kijiji ujuzi, mazoea na tabia vilivyosababisha mradi mdogo wa msaada kufanikiwa kama katika kijiji cha sauri, Kenya,ambako Jeffrey Sachs yupo na kuifanya kuwa ndio hali ya kila mtu
misaada inaongeza rasilimali kwa serikali na hiyo inasababisha kufanya kazi serikalini kuwa na faida utakuta mtu Afrika anatafuta ajira kwa kuongeza ushawishi wa kisiasa wa serikali na hasa katika jamii zetu zenye makabila mbalimbali misaada inachochea misuguano ya kikabila kwa kuwa kila kabila litakuwa linataka kuingia serikalini ili liweze kupata sehemu ya misaada mabibi na mabwana,watu wenye ujuzi zaidi Afrika hawapati fursa za kufanya kazi na biashara na sekta binafsi kwa kuwa sera zilizopo hazivutii biashara serikali hazitaki kubadilisha hali hii, Kwa nini? kwa sababu hawahitaji kuongea na wananchi wao. wanaongea na mashirika ya misaada ya kimataifa kwa hiyo waafrika wenye ujuzi zaidi wanaishia kufanya kazi serikalini na hiyo imeongeza misuguano ya kisiasa katika nchi zetu kwa kuwa tunategemea misaada
nataka kusema pia ni muhimu kwetu kukumbuka kuwa kwa miaka 50 iliyopita Afrika imekuwa ikipokea misaada inayozidi kuongezeka kutoka kwa jamii ya kimataifa katika njia za misaada ya kiufundi na fedha na katika njia nyingine za misaada kati ya mwaka 1960 na 2003 bara letu lilipokea dola billioni 600 za misaada na bado tunaelezwa kuwa kuna umaskini mwingi katika bara la afrika misaada yote hii imeenda wapi?
nataka kutumia mfano wa nchi yangu mwenyewe ya Uganda jinsi misaada ilivyoleta mfumo wa utegemezi Katika bajeti ya 2006-2007,makisio ya mapato yalikuwa ni 2.5 trillion shillings makisio ya misaada ilikuwa ni 1.9 trillion. Matumizi ya Uganda yanayojirudi rudia,ninaposema hivi ninamaanisha nini? ninamaanisha kutoka mkononi kwenda mdomoni ni trillioni 2.6 Kwa nini bajeti ya serikali ya Uganda inatumia asilimia 110 ya mapato yake? kwa sababu kuna mtu anayeitwa misaada anayeichangia Lakini hii inakuonyesha kuwa serikali ya Uganda haijajifunga kutumia mapato yake yenyewe kuwekeze katika uzalishaji Lakini inatumia mapato haya kulipia matumizi ya sekta ya umma usimamizi wa serikali ambao ni wa kujuana sana,unachukua billioni 690 Jeshi, billioni 380 Kilimo ambacho kinaajiri asilimia 18 ya watu wetu ambao wengi ni maskini kinachukua billioni 18 tu. Viwanda na biashara vinachukua billioni 43 Ngoja nikuonyeshe ni nini matumizi ya umma matumizi ya usimamizi wa umma yana nini ndani yake? mawaziri 70, washauri wa rais 114 ambao hawaonani na rais, isipokuwa katika runinga
na pale wanapokutana naye ni katika shughuli za kijamii kama hii, na hata hapo ni yeye anayewashauri
tuna serikali za mitaa 81 kila moja imeundwa kama serikali kuu watawala, baraza la mawaziri, bunge na kazi nyingine nyingi kwa washirika wa kisiasa zilikuwa 56,na pale rais wetu alipotaka kubadilisha katiba ili kuondoa ukomo wa kutawala aliunda wilaya mpya 25, na sasa kuna wilaya 81 wabunge 333 unahitaji uwanja cha wembley kuweza kufanya kikao cha bunge letu tume 134 na vyombo vya serikali vyenye uhuru usio kamili vyote vikiwa na wakurugenzi na magari, na kitu cha mwisho hii naielekeza kwa Ndugu Bono. katika kazi yake anaweza akatusaidia katika hili
utafiti wa karibuni wa serikali ya Uganda uligundua kuwa kuna magari ya kifahari 3000 katika makao makuu ya waziri wa afya Uganda ina tarafa 961,kila moja ikiwa na kituo cha afya lakini hakuna hata kimoja chenye gari la kubebea wagonjwa kwa hiyo magari ya kifahari makao makuu yanawaendesha mawaziri,makatibu wa wizara,viongozi viongozi kutoka mashirika ya misaada wanaofanya katika miradi ya misaada wakati maskini wanakufa kwa kukosa magari ya wagonjwa na madawa
Mwisho,nataka kusema kuwa kabla ya kuja hapa kuzungumza niliambiwa kuwa msingi wa TEDGlobal ni kuwa hotuba nzuri inatakiwa iwe kama sketi fupi inatakiwa iwe fupi kiasi cha kuamsha hisia lakini pia ndefu kufunika jambo lenyewe natumaini nimefanikisha hilo
You can share this video by copying this HTML to your clipboard and pasting into your blog or web page. This video will play with subtitles.
You either have JavaScript turned off or have an old version of the Adobe Flash Player. To view this rating widget you
need to get the latest Flash player.
If your browser allows only "trusted sites" to execute Javascript, you should add the "googleapis.com" domain to your whitelist to allow our Flash detection to work properly.
Got an idea, question, or debate inspired by this talk? Start a TED Conversation.
katika maongezi haya, mwandishi wa habari Andrew mwenda anatuambia kubadilisha "swali kuhusu Afrika" kuangalia zaidi ya habari za umaskini, vita na hali ya kushindwa kujisaidia, na kuona fursa za kutengeneza ustawi na furaha katika kila eneo barani.
Journalist Andrew Mwenda has spent his career fighting for free speech and economic empowerment throughout Africa. He argues that aid makes objects of the poor -- they become passive recipients of charity rather than active participants in their own economic betterment. Full bio ยป
Translated into Swahili by Joachim Mangilima
Reviewed by Hector Mongi
Comments? Please email the translators above.
22:10 Posted: Jul 2007
Views 275,348 | Comments 99
18:23 Posted: Aug 2007
Views 330,993 | Comments 90
17:50 Posted: Jul 2007
Views 282,951 | Comments 85
Just follow the guidelines outlined under our Creative Commons license.
This comment will be attributed to . Not ? Sign Out.